Category: Siasa
Matakwa ya Rwanda yasiivunje EAC
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umezorota. Uhusiano huo umezorota baada ya matukio mawili. Tukio la kwanza ni ushauri Rais Jakaya Kikwete aliompa Rais Paul Kagame wa kuzungumza na waasi wa kundi la FDLR kwa nia ya kurejesha amani. La pili ni Tanzania kupeleka majeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na waasi wa M23.
Sasa ianzishwe Mahakama ya dawa za kulevya, ujangili
Vita dhidi ya dawa za kulevya inahitaji msukumo, mbinu na sheria mpya. Hii si vita ya Polisi, Usalama wa Taifa wala Serikali pekee. Wala vita hii hatuwezi kuishinda kwa kubaki tukioneana haya au tukiogopana.
Kwa wiki kadhaa, vyombo vya habari, tukiwamo sisi JAMHURI, tumeamua kwa dhati kabisa kuishiriki vita hii. Tumefanya hivyo kwa kutambua madhara makubwa yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana wetu.
Kamati Kuu CCM ikomeshe mgogoro unaofukuta Bukoba
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanajipanga kukutana wiki hii kutafuta ufumbuzi wa mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera. Imeshadhihirika wazi kuwa mgogoro huo ni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Meya Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.
Wezi wa fedha za Smart Partnership washitakiwe
Kwa wiki kadhaa gazeti la JAMHURI tumeandika habari za ufisadi wa mamilioni ya shilingi kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue).
Rais JK, orodha ya mapapa wa mihadarati imeyeyukia wapi?
Katika gazeti hili kuna barua iliyoandikwa na mmoja wa Watanzania walio kwenye magereza Hong Kong, kutokana na usafirishaji mihadarati.
Matusi kwa Rais wetu hayakubaliki
Kwa muda sasa, kumekuwapo maneno mengi kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda yakimlenga Rais wetu, Jakaya Kikwete. Chanzo cha yote haya ni mapendekezo ya Rais Kikwete ya kumwomba Rais Kagame aketi na waasi wa kundi la FNBL ili kukomesha mapigano na mauaji yanayoendelea Rwanda na upande wa mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).