JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Haya ndiyo mambo murua yanayoliliwa na Watanzania

Wizara ya Nishati na Madini imetangaza kupunguza gharama za kuunganishia wateja wake umeme. Gharama hizo zimepungua kwa wastani wa asilimia 30 na 77. Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, bungeni mwishoni mwa wiki.

Wabunge, Nishati acheni mivutano

 

Ijumaa wiki hii Wizara ya Nishati na Madini inatarajiwa kuwasilisha bajeti yake bungeni. Kama ilivyo kawaida tayari harakati zimeanza. Wabunge wanapigana vikumbo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco William Mhando amesimamishwa kazi na Wizara ya Nishati na Madini  inapambana na upatikanaji wa umeme.

Tuache kasumba ya kupuuza kila linalozungumzwa na Wapinzani

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, amezungumza mambo mazito mno mwishoni mwa wiki. Sehemu ya hotuba yake tumeishapisha neno kwa neno ndani ya gazeti hili.

Tuwe makini kulinda ardhi yetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, jana aliwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya mwaka 2012/2013.

Mchechu NHC ameonyesha njia, wakurugenzi wengine mko wapi?

Wiki iliyopita Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepata mkopo wa wastani wa Sh bilioni 165. Shirika limeupata mkopo huu kutoka benki na mashirika tisa ya fedha. Mashirika na benki zilizotoa mkopo huu na kiasi cha fedha walizotoa kwenye mabano ni CRDB Bank (Sh 35 bilioni), ECO Bank (Sh 20 bilioni), ABC (Sh 4 bilioni), NMB (Sh 26 bilioni), CBA (Sh 24 bilioni), TIB (Sh 22 bilioni), Azania (Sh 7 bilioni), Local Authorities Pension Fund-LAPF (Sh 15 bilioni) na Shelter Africa Company (Sh 22 bilioni).

 

Bila reli, barabara zitakufa

Wizara ya Ujenzi, kama zilivyo wizara nyingine, ni miongoni mwa wizara chache ambazo ni mihimili ya maendeleo ya taifa letu.

Tanzania, tofauti na makoloni mengine, iliachwa na watawala dhalimu ikiwa haina barabara, si za lami tu, bali hata za changarawe.