JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Michezo

Haya ndiyo maajabu ya ‘fair play’ kwenye soka

Mashabiki 114,580 walishuhudia Ali Bin Nasser kutoka Tunisia akirudi katikati ya dimba baada ya kupuliza filimbi katika dakika ya 51 kwenye Uwanja wa Azteca Juni 22, 1986 nchini Mexico, katika mchezo wa robo fainali Kombe la Dunia kuruhusu bao la…

Kwaheri De Gea, karibu Mkwasa

Ni mkono wa kwa heri kila kona; huku tunaagana na Mart Nooij kule katika Jiji la Manchester, ambalo linakuwa na anga nyekundu mara bluu, kuna kuagana na David De Gea. Presha imekuwa kubwa na haizuiliki tena watu kurudi katika asili…

Ya TFF na Mayweather

Ilikuwa ni mkesha wa hiari kusubiri pambano la masumbwi kati ya Mmarekani Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililoacha gumzo kwenye ulingo mmoja maarufu pale Las Vegas, Marekani. Wapo waliolala kwa mang’ang’amu kusubiri pambano hilo na wengine kukesha. Kulikuwa na mabishano…

Messi wa Simba kortini, Messi wa Barca dimbani

Ninapotazama soka hapa nchini, nawaona wachezaji wetu ni kama yatima kutokana na mfumo wa ukuzaji wa vipaji wa nchi, kadhalika ni wa kujitakia. Kuna kitu kikubwa wachezaji wetu wanachokosa, wamekuwa ni watu wanaojipa majukumu mazito kwa kutokujua au ubinafsi tu. Mchezaji…

Fasta fasta inavyoumiza michezoni

Wahenga walinena “haraka haraka haina baraka” tena wakanena “mwenda pole hajikwai.” Wahenga pia walitambua kuwa kwenye dharura haraka inaweza kutumika ndiyo maana wakanena pia “ngoja ngoja yaumiza matumbo.”  Tunajua vyema kuwa dharura huwa haidumu, na jambo la mara moja linatatuliwa…

Kule Fellain, huku Makapu

Kuna wakati ili ufanikiwe basi ni vyema kujifunza kwa yule aliyefanikiwa. Mtu aliyefanikwa kwa kumwangalia tu matendo yake unapata funzo. Unaweza kumwangalia namna anavyoongea, anavyotembea, anavyocheka na namna anavyochagua marafiki, kusikiliza watu na kadhalika na utajikuta umepata funzo kubwa sana…