Category: Kitaifa
Bunge lamkaanga JK
*Kura ya kutokuwa na Imani ni kikombe cha shubiri
*Wabunge wanajipanga kupata kura 176 kumwadhibu
*Spika wa Bunge ameahirisha tatizo, Zitto aibuka shujaa
WIKI iliyomalizika ilikuwa ni ya msukosuko wa hali ya juu baada ya Bunge kuamua kumkaanga Rais Jakaya Kikwete kupitia mgongo wa mawaziri wake.
Mabwawa ‘hewa’ ya Sh milioni 720 yachimbwa
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisitofautiane na wenzangu wote waliozungumza.
Mbunge: Wezi fedha za umma wanyongwe
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Mohamed (CCM), ni miongoni mwa wabunge waliochangia na kulaani vikali matumizi mabaya ya fedha za umma na hujuma zinazofanywa na viongozi.
Serikali: Vitambulisho vya uraia vinatolewa bure
SERIKALI imewatoa hofu wananchi kwa kuwahakikishia kuwa vitambulisho vya uraia vitatolewa bure kwa Watanzania wote. Msimamo wa Serikali ulitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge.
Bosi TBS hachomoki
*CAG aanika madudu mengine mapya
*Omo, Blueband, mafuta ya ndege hatari
*Pikipiki feki, vinywaji hatari kwa walaji
*Aruhusu Kobil wachakachue mafuta
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametoa taarifa ya ukaguzi maalumu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kuibua mambo ya hatari zikiwamo kampuni za mawaziri zinazoingiza mafuta ya magari yasiyofaa.
Wakubwa wanavyotafuna nchi
[caption id="attachment_27" align="alignleft" width="314"]Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utoah, akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2009/2010 kwa waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, wiki iliyopita[/caption]*Kampuni ya Mohamed Enterprises yauziwa viwanja kinyemela
*Bandari watumbua zaidi ya bilioni 1.5, waendesha miradi hewa
*Mabosi wanachomeka watumishi hewa, wanavuta mishahara
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2011; imeendelea kufichua namna kundi la watumishi wa umma na wafanyabiashara wakubwa wanavyoitafuna Tanzania. Utouh aliwasilisha taarifa hiyo bungeni mwishoni mwa wiki.