JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

Mkulo alivyopiga dili

[caption id="attachment_46" align="alignleft" width="314"]Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji akiteta na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Mchemba[/caption]*Siri nzito zavuja alivyoishinikiza CHC iwauzie kiwanja Mohammed Enterprises
*Katika kumlinda Katibu Mkuu akanusha maelekezo aliyotoa Mkulo hotelini
*Soma mgongano wa kauli na nakala za mashinikizo ya Wizara ya Fedha kwa CHC

Siri nzito na zenye kuitia aibu Serikali juu ya mgogoro wa uuzaji wa kiwanja Na. 10 kilichopo Nyerere Road kwa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) zimeanza kuvuja.

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Jamhuri kwa wiki tatu sasa na kufanikiwa kupata nyaraka nzito kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), zinafanana kwa kila hali na nakala ya nyaraka zilizopo Wizara ya Fedha, unashitua.

Vincent Nyerere alivyoilipua TBS bungeni

Katika Mkutano wa Bunge uliomalizika, Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), alilipua mbinu zilizofanywa na ‘wakubwa’ wa TBS kwa kujiundia kampuni hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi na kuliibia taifa mabilioni ya shilingi. Yafuatayo ni maneno aliyoyazungumza bungeni.

EWURA yazidi kubana wachakachuaji

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mafuta na Maji (EWURA) sasa imepiga hatua nyingine na kufanikiwa kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ya dizeli na petroli, baada ya kuanza kutumia teknolojia ya vinasaba (maker).

Bunge lamkaanga JK

*Kura ya kutokuwa na Imani ni kikombe cha shubiri
*Wabunge wanajipanga kupata kura 176 kumwadhibu
*Spika wa Bunge ameahirisha tatizo, Zitto aibuka shujaa

WIKI iliyomalizika ilikuwa ni ya msukosuko wa hali ya juu baada ya Bunge kuamua kumkaanga Rais Jakaya Kikwete kupitia mgongo wa mawaziri wake.

Mabwawa ‘hewa’ ya Sh milioni 720 yachimbwa

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisitofautiane na wenzangu wote waliozungumza.

Mbunge: Wezi fedha za umma wanyongwe

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Mohamed (CCM), ni miongoni mwa wabunge waliochangia na kulaani vikali matumizi mabaya ya fedha za umma na hujuma zinazofanywa na viongozi.