Category: Kitaifa
Ikulu kukarabatiwa kwa Sh bilioni 6
Wabunge kadhaa wamejiandaa kuhoji matumizi ya Sh bilioni 6 zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu. Kiasi hicho cha fedha kimetengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013. Wabunge wanahoji kiasi hicho kikubwa hasa kutokana na kuonekana kuwa kila…
RUSHWA BUNGENI
*Halmashauri Dar zawahonga mil. 25/-
*Mbunge CCM asema Chadema ‘inawaovateki’
Kamati ya Kudumu y Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inatajwa kuwa miongoni mwa kamati zinazonuka rushwa, na kuna habari kwamba wabunge wengine watatu wataunganishwa na mwenzao katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa.
NIDA yataja faida za vitambulisho
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeamua kutoa elimu kwa wananchi, katika mchakato wa kutoa vitambulisho vya uraia kwa Jiji la Dar es Salaam unaotarajiwa kuanza wakati wowote mwanzoni mwa mwezi huu.
Kwa msimamo huu wa SMZ Muungano hauponi (1)
Mada hii ilitayarishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, na kuwasilishwa katika Mkutano Maalumu ulioandaliwa na Zanzibar Law Society Kuadhimisha Miaka 41 ya Muungano. Ulifanyika katika Hoteli ya Bwawani, Zanzibar mnamo Aprili 23, 2005. Ukisoma aya moja baada ya nyingine, utaona tofauti ndogo mno katika misimamo ya Uamsho na SMZ. Lililo wazi ni kwamba Muungano unakabiliwa na kifo. Endelea…
Bila kumpata Kagame wetu tutakwama
Nilipata kusoma makala ya kiongozi wangu wa kitaaluma, Jenerali Ulimwengu, akikosoa Watanzania wenye matamanio ya kumpata ‘Kagame’ wao.
Mzimu uliowanyoa mawaziri unahitaji tambiko—2
Wiki iliyopita nilibainisha kuwa kiini cha tatizo la ufisadi wa nchi hii inaonekana hakijabainika; ndiyo maana tunahangaika na matokeo badala ya kiini.