Category: Kitaifa
Twende tuwekeze Sudan Kusini – Jenerali Kisamba
*Saruji, ngano, vifaa vya ujenzi, alizeti vinahitajika *Asema majirani zetu wameshaanza kunufaika mno Ushauri umetolewa kwa Tanzania na Watanzania kuamka na kuchangamkia fursa za uwekezaji na biashara zilizojitokeza katika taifa jipya la Sudani Kusini. Ushauri huo umetolewa na…
Kashfa uporaji ardhi kubwa Pinda ahusishwa
*Mmoja wa washirika ajitoa kuepuka aibu
*Ni Chuo Kikuu cha Iowa cha Marekani
*Yabainika wanaleta teknolojia hatari nchini
[caption id="attachment_124" align="alignleft" width="160"]Waziri Mkuu Mizengo Pinda[/caption]Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameendelea kubanwa kuhusu uamuzi wake wa kuwasaidia Wamarekani kujitwalia ekari laki nane za ardhi kwa miaka 99 mkoani Katavi.
Nyalandu anavyomhujumu Kagasheki
*Adaiwa kula njama wawekezaji wasilipe kodi
*Aendesha kikao bila Kagasheki kuwa na taarifa
*Bodi ya TANAPA yakataa mapendekezo yake
Mgogoro ulioripotiwa na Gazeti hili la JAMHURI wiki iliyopita kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheni na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, sasa umechukua sura mpya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu, ameingia matatani tena baada ya kubainika kuwa anashinikiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) lisianze kutoza ‘concession fee’ katika hoteli za kitalii nchini, JAMHURI limebaini.
Uamuzi huo unaikosesha Serikali mapato yanayofikia Sh bilioni 17 kwa mwaka. Jaribio la kwanza la Nyalandu kufanikisha mpango wake liligonga mwamba kwenye kikao chake na menejimenti ya TANAPA, kilichofanyika Juni 8, mwaka huu mjini Moshi.
Pinda akunjua makucha rasmi
Serikali imesema kuanzia sasa watumishi wabadhirifu wa fedha za umma hawatahamishiwa vituo vingine vya kazi, bali watachunguzwa na ikibainika watafukuzwa kazi mara moja.
Katibu Mkuu Nishati amwagiwa sifa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, amemwagiwa sifa kwa jinsi alivyowabana watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kufanikisha upatikanaji wa mita 85,000 za umeme.
Mawaziri wagombana
*Naibu Waziri adaiwa kumhukumu Kagasheki wizarani
*Atajwa kutoa matamshi ya kumkejeli huko TANAPA
*Waziri asema atamhoji, yeye asema wanawachonganisha
[caption id="attachment_112" align="alignnone"]Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kagasheki akiwa na Naibu wake, Lazaro Nyalandu kabla hali ya hewa haijachafuka[/caption]
MGOGORO mzito unafukuta ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo sasa kuna msuguano mkali kati ya Waziri Khamis Kagasheki na Naibu wake, Lazaro Nyalandu.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Wizara hiyo, zinasema kuwa Kagasheki amepata taarifa kutoka kwa baadhi ya watendaji waliokuwa na watu mbalimbali walikuwa Arusha kwenye kikao alichokiendesha Nyalandu kati yake na maafisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), alipomkejeli Kagasheki hivi karibuni.
“Katika Mkutano huo, Nyalandu alipoulizwa na wafanyakazi wa TANAPA juu ya hatua ya Waziri Kagasheki kusimamisha watumishi wanne wa TANAPA na askari 28, alisema ‘Waziri alikurupuka.’ Alisema ‘kama Waziri angeshauriana na yeye (Nyalandu) wala asingewasimamisha wafanyakazi hao,” kilisema chanzo chetu.