Category: Kitaifa
Serikali yaelekea kukubali hoja ya Waislamu
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaelekea kulikubali ombi la kundi la waumini wa Kiislamu wanaotaka dodoso la dini liingizwe kwenye Sensa ya Watu na Makazi iliyopangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu.
Uamuzi huo ambao umeshawahi kupingwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa, unatajwa kwamba huenda ukatangazwa hivi karibuni baada ya ngazi ya juu ya uongozi “kutafakari” na kubaini kuwa dodoso hilo haliwezi kuathiri umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWA PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2012/13
Muhongo, Maswi wanatisha
*Gharama za kuunganisha umeme zakuna wengi
*Migodi yote si hiari tena kulipa kodi ya mapato
*Afuta mashangingi ya bure, vigogo watakopeshwa
*Mnyika, Selasini wawanyoosha wabunge wala rushwa
Wananchi wengi wameeleza kufurahishwa na msimamo wa uongozi mpya wa Wizara ya Nishati na Madini wa kuwapunguzia wananchi ukali wa gharama za kuunganisha umeme, kufuta ununuzi wa mashangingi na kuwabana wenye migodi mikubwa kuanza kulipa kodi ya mapato.
Vita kubwa TANESCO
*Wabunge wajiandaa kukwamisha tena bajeti ya Wizara ya Nishati, wahoji zabuni ya mafuta BP
*Wajiandaa kuwang’oa Waziri Profesa Muhongo, Katibu Mkuu Maswi Ijumaa ya wiki hii
*Katibu Mkuu aanika ukweli, asema Wizara yake haikufanya manunuzi waliohusika ni RITA, Zitto anena
[caption id="attachment_219" align="alignleft" width="243"]Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo[/caption]Kuna kila dalili kuwa imeibuka vita ya wazi kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, William Mhando, akipigiwa debe la wazi na wabunge.
Taarifa zilizopatikana kwenye ofisi za Bunge zinasema kuwa Kamati ya Nishati na Madini inajipanga kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, Injinia Mhando, hatarejeshwa kazini huku wizara ikisisitiza kuwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wala hajafukuzwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, naye ana msimamo kuwa Mhando ameonewa na wizara inaweza kujiokoa kwa kumrejesha ofisini kisha ufanywe uchunguzi maalumu utakaoendeshwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Ufisadi watikisa Bunge
*Unahusu kada wa CCM anayechimba urani
*Profesa Tibaijuka amtwika mzigo Jaji Werema
*Naibu Spika aagiza Waziri Muhongo ajiandae
*Sinema nzima imeibuliwa na Halima Mdee
Wafanyabiashara ndugu wanaodaiwa kubadili matumizi ya ardhi kutoka uwindaji wa kitalii na kuanza harakati za uchimbaji madini ya urani, wameibua mgongano mkubwa bungeni na serikalini. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amemwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, asaidie kupata utatuzi kashfa hiyo.
Hotuba ya Lissu iliyolitikisa Bunge, Serikali
*Atoboa siri majaji wengi ‘vihiyo’, washindwa kuandika hukumu
*Aeleza namna wakuu wa wilaya walivyoteuliwa kwa rushwa
*Yumo mwingine aliyehukumiwa kwa ubaguzi wa ukabila
Ifuatayo ni sehemu ya maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kuhusu Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013. Lissu alitoa maoni haya na kwa kiasi fulani yaliibua mjadala mkali bungeni, huku Serikali ikitaka aondoe baadhi ya maneno, na yeye akakataa. Endelea…
UTEUZI WA MAJAJI
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua ukweli kwamba Rais Kikwete ameteua majaji wengi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kuliko marais wengine wote waliomtangulia kwa ujumla wao. Rekodi hii peke yake inaonyesha kwamba Rais anatambua umuhimu wa Mahakama Kuu kuwa na watendaji wa kutosha wa utoaji haki ili kutekeleza dira ya ‘haki kwa wote na kwa wakati.’