JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

Majaji maji shingoni

*Maelezo ya Jaji Ramadhani, Luanda moto

*Ripoti ya Ikulu nayo yataka waondolewe

*Lissu ataka wapime, kumshitaki Kikwete

*Amtaka Jaji Kiongozi Fakih Jundu ajiuzulu

 

Mhimili wa Mahakama umetikisika baada ya kuwapo ushahidi wa wazi kwamba Rais Jakaya Kikwete amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa kuwaongezea mikataba ya kazi baadhi ya majaji na kumpandisha cheo mwingine.

RIPOTI MAALUMU

Majaji ‘vihiyo’ watajwa

*Yumo aliyeshindwa kuandika hukumu miaka minne

*Wengine wagonjwa, hawajawahi kusikiliza kesi

*Yumo Jaji wa Mahakama ya Rufaa asiye na shahada

*Baada ya kubanwa sasa anasoma Chuo Kikuu Huria

*Wengine walikuwa mahakimu watuhumiwa wa rushwa

 

Wabunge waunga mkono msimamo wa Morocco

Bunge la Tanzania linaunga mkono msimamo wa Morocco katika kupata ufumbuzi wa mgogoro kati ya taifa hilo na taifa la Sahara Magharibi. Mwaka 1975 uliibuka mgogoro wa ndani kati ya Morocco na taifa la Sahara Magharibi linalotaka kujitangazia Uhuru. Mgogoro huu uliofanya Sahara Magharibi kujenga ukuta kama wa Berlin kule Ujerumani, umekuwa na madhara makubwa ndani ya taifa la Morocco.

Malawi waigwaya kipigo JWTZ

* Taarifa za kiintelejensi za Jeshi letu zawaogopesha

* Ndege za utafiti zaondolewa upande wa Tanzania

* Makamanda wasisitiza kuendelea kuulinda mpaka

* Waingereza walipotosha mpaka

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaendelea kuimarisha ulinzi katika mpaka wa Tanzania na Malawi, licha ya taifa hilo dogo lililopo kusini mwa Afrika kuonyesha nia ya kutotaka kuingia katika vita, lakini pia gazeti la JAMHURI limebaini chimbuko la historia ya upotoshaji katika mpaka wa nchi hizi.

JWTZ wasogea mpakani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe, ameionya Serikali ya Malawi kuhusu mgogoro wa mpaka, katika kile kinachoonekana kuwa Tanzania ipo tayari kuingia vitani endapo itapuuzwa. Wakati Membe akitoa msimamo huo mkali bungeni jana, kuna habari kwamba wanajeshi na vifaa vya kijeshi wameshapelekwa karibu na eneo la mgogoro ajili ya kuimarisha ulinzi.

Dk. Lwaitama: Serikali tatu hazikwepeki

 

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavel Lwaitama (pichani), amesema suluhisho pekee la kunusuru Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwa na Serikali tatu.

Dk. Lwaitama alitoa kauli hiyo katika Mazungumzo ya Asubuhi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania na kufanyika katika Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam jana.