JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

‘Kikitokea chama kama CCM ya Nyerere kitatawala milele’

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alidhamiria kuifanya Tanzania kuwa paradiso.

“Mwalimu alitaka kujenga paradiso ya hapa duniani katika nchi hii. Kama tungetekeleza misingi aliyotuwekea, Tanzania ingekuwa paradiso.” Haya ni maneno ya Ibrahim Kaduma (75).

Kaduma ameshika nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za ukurugenzi na uwaziri katika Serikali ya Awau ya Kwanza.

‘Dokta Nchia’: Mpishi wa Nyerere

*Asema Mwalimu alipofungwa bao hakula

“Dokta Nchia”, kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyopenda kumuita, hakuwa daktari wa binadamu au mifugo. Alikuwa daktari wa mlo.

Simulizi ya mjukuu wa Mwalimu Julius kambarage Nyerere

*Amepata kuswekwa rumande kwa kuendesha trekta

Petro John Nyerere ni mmoja wa wajukuu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Baba yake ni John Guido Nyerere, mtoto wa nne wa Baba wa Taifa. Petro ni mmoja wa wajukuu wachache kati ya wengi walioishi muda mrefu na babu yao pamoja na bibi yao, Mama Maria Nyerere.

Anna Mwansasu: Walitaka kumwekea Nyerere damu ya Wazungu

Miaka 13 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, afariki dunia, waliokuwa wasaidizi wake wa karibu bado wana kumbukumbu ya mambo mazito kuhusiana na ugonjwa uliosababisha kifo chake. Si hilo tu, Serikali nayo imewasusa na wengi wanaishi maisha ya tabu haijapata kutokea. Yafuatayo ni mahojiano kati ya JAMHURI na Anna Mwansasu, aliyekuwa Katibu Muhutasi wa Mwalimu Nyerere…

Rais Nyerere alipokosa maji ya kuoga Kibondo

Mwaka 1964, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Tanganyika, alitembelea shule yetu.  Nilikuwa nasoma Seminari ya Kaengesa Sumbawanga. Bendi ya shule yenye vyombo vyote vya brass band tulimpigia wimbo maarufu uitwao “The Washington Post”.

Siri kifo cha Nyerere

Juhudi za chini chini zimeanza kufanywa na baadhi ya Watanzania ambao hawajaridhika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifariki kifo cha kawaida.