Category: Kitaifa
NSSF: Fao la kujitoa ni hatari
*Wananchi, Serikali wahadharishwa
*Machafuko ya kiuchumi yatatokea
*Yasema ikiamuriwa ina fedha za kulipa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) halijachoka kuwaasa Watanzania na Serikali juu ya athari za kutekelezwa kisheria kwa fao la kujitoa.
Dar es Salaam mpya
*NSSF kuanzisha miradi mikubwa jijini
*Mizigo bandarini kuondolewa kwa treni tano
*Mwisho wa malori kuingia jijini wawadia
*Nyumba zote Manzese, Vingungu kuvunjwa
Sura ya Jiji la Dar es Salaam itabadilishwa na kugeuka jiji la kisasa ndani ya miaka minne ijayo kutokana na mpango mzito ulioandaliwa na Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF).
…Mnyika: Chadema ngoma nzito
*Asema Chadema ina baraka za Mwalimu Nyerere
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetamba kwamba nguvu yake haitamalizwa na ziara za viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mikoani, katika kipindi hiki ambacho Watanzania wengi wanahitaji mabadiliko.
JK kikwazo CCM
*Yabainika ndiye mwasisi wa makundi CCM
*Akemea dhambi iliyomwingiza madarakani
Staili ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete, inatajwa kwamba haitakuwa na msaada mkubwa wa kuiwezesha Sekretarieti mpya kutekeleza ahadi na maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane uliomalizika mjini Dodoma hivi karibuni.
Urais ni Magufuli, Membe, Lowassa
*Wasira, Mwakyembe, January Makamba nao watajwa kundini
Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliomalizika mjini Dodoma wiki iliyopita, umetoa ishara ya baadhi ya wanachama wanaoweza kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wazungu Mererani wasalimu amri
Kampuni ya TanzaniteOne Ltd inayochimba madini ya tanzanite katika eneo la Mererani mkoani Manyara, hatimaye kuanzia wiki hii italazimika kuachia asilimia 50 ya hisa zake zimilikiwe na wazalendo, imethibitishwa.