Category: Kitaifa
Medeye afichua siri migogoro ya ardhi Arumeru
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gooluck ole Medeye (CCM), ameibuka na kuanika siri ya migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.
Lissu, Mrema, Mbowe wamsulubu Kikwete
[caption id="attachment_693" align="alignleft"]Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu[/caption]*Wasema nchi imemshinda, watapika nyongo
*Wasema Serikali inaandaa taifa la wajinga
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Tanzania Labor Party (TLP), Agustino Mrema, wametoa tuhuma nzito kuwa nchi imemshinda Rais Jakaya Kikwete.
Kasi yetu ya kuchimba dhahabu inatisha, idhibitiwe
Mikataba ya kuchimba dhahabu hapa nchini ilianza kusainiwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Mzee Benjamin William Mkapa.
Silaa: Nawakilisha vijana CC
Msatahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amesema anamshukuru Mungu, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), kwa kumchagua kwa kishindo kuingia katika Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.
Mgiriki aiweka ‘Serikali’ mfukoni
*Aingia Selous kuua wanyamapori
Raia wa Ugiriki, Pano Calavrias, aliyeghushi uraia wa Tanzania na kisha kuhukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mwaka 2010 kwa kosa la kukutwa na hati ya kusafiria ya Tanzania kinyume cha sheria, yupo nchini akiendelea na uwindaji wa kitalii.
Mgogoro mpya CCM
*Viongozi waendelea kufitiniana kupata urais, ubunge 2015
*Kinana aonya, akemea wabunge wasiokwenda majimboni
*Aikubali hoja ya Dk. Slaa, ataka wawekezaji feki watimuliwe
*Ataka wagombane kuboresha maisha ya watu si kuingia Ikulu
Mgogoro mpya wenye sura ya kuwania madaraka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama uliotokea mwaka 2007 ukaivunja Serikali, sasa unafukuta upya katika hatua tatu tofauti, JAMHURI imebaini.