Category: Kitaifa
Walimu wapya 53 hawajaripoti Kasulu
Wakati tarehe ya mwisho ya walimu wapya kuripoti katika shule walizopangiwa kufundisha ni Machi 9, mwaka huu, kama ilivyotangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, walimu 53 kati ya 329 hawajaripoti katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma.
Lowassa ajiimarisha bungeni
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amezidi kujiimarisha kisiasa baada ya kuongeza idadi ya wenyeviti wa Kamati za Kisekta za Bunge wanaomuunga mkono.
Wakataa maji wakidai hawakushirikishwa
Wakazi wa Kitongoji cha Mkulila, Kijiji cha Wambishe wilayani Mbeya, wamekataa mradi wa umwagiliaji maji waliopelekewa na Serikali, wakidai hawakushirikishwa katika uanzishwaji wake.
Kibanda alivyotekwa
Mfanyakazi wa Kampuni Ikolo Investiment Ltd, Joseph Ludovick (31), aliyekamatwa na Polisi akihusishwa kwenye sakata la utekaji na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, anatajwa kuwa ni mtu muhimu katika upelelezi wa tukio hilo.
Haki za wanawake zitambuliwe kwenye Katiba
Haki ya mwanamke ni suala linalohitaji kupewe umuhimu wa kipekee katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ujasiriamali waajiri vijana 3,000 Arusha
Wahitimu zaidi ya 3,000 wa mafunzo ya ujasiriamali katika taasisi ya The Fountain Justice Training College ya jijini Arusha, wameweza kujiajiri na hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.