Category: Kitaifa
Rwanda: Kagame hakumtukana Kikwete
*Yawataka Watanzania kupuuza uvumi mitandaoni
Baada ya kuwapo joto kali la maneno ya kidiplomasia kutoka kwa maafisa wa Serikali za Tanzania na Rwanda kutokana na habari kwamba Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemtukana Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Serikali ya Rwanda sasa imetoa msimamo rasmi kukanusha tuhuma hizo.
Chikawe: Tume ya Katiba ipokee maoni, isijibu
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe ameitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba kusikiliza zaidi maoni ya wananchi na kuyapokea badala ya kuyajibu kila yanapotolewa.
Madiwani Chadema Geita wafichua ufisadi wa bil 11/-
*Tamisemi, Hazina, CCM wahusishwa
Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Halmashauri ya Mji wa Geita, kwa kushirikiana na mmoja wa Viti Maalum wa Halmshauri ya Wilaya ya Geita, wametoa nyaraka katika mkutano hadhara uliofanyika Julai 14, mwaka huu, zinazoonesha wilaya hiyo kupokea Sh bilioni 11 kwa ajili ya ununuzi wa madawati lakini matumizi yake hayajulikani.
Wasira: Nivigumu kuifuta Chadema
*Akiri kuwa kazi hiyo si nyepesi
Kukifuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) si rahisi; amethibitisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira.
Wanaume watelekeza watoto walemavu Arumeru
*Wanawake wasukumiwa mzigo
Tatizo la wanaume kuwatelekeza watoto wao wenye ulemavu, limetajwa kukithiri katika Kijiji cha Ambureni, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.
Ulaji ugeni wa marais 11
Kampuni ‘hewa’ zakomba mamilioni
*CAG atakiwa aingie kazini mara moja
Kampuni tatu kati ya nane zilizozawadiwa zabuni tata za vifaa na huduma kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue), zimebainika kuwa ni ‘hewa’.