Category: Kitaifa
Majaji wanaolinda wauza ‘unga’ wabainika
>>Gazeti hili sasa limeamua kuwataja kwa majina
>>Mahakimu nao wanawaachia mapapa kienyeji
>>Kigogo ofisi ya DPP, Mahakama Temeke, Kinondoni ni balaa
Mahakama kupitia baadhi ya majaji na mahakimu wasio waadilifu imebainika kuwa kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.Pamoja na Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP), nayo imelaumiwa kwa kufuta kesi katika mazingira ambayo hata mtu ambaye hakusoma sheria, anaweza kuyatilia shaka.
Wakati vyombo hivi vikikwamisha vita hii, lawama zimekuwa zikielekezwa kwa polisi na vyombo vingine vya usalama, ambavyo watendaji kazi wake wanafanya kazi usiku na mchana.
Waasi M23 wachapwa Goma
Brigedi ya Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) inayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, imewadhibiti waasi wa kundi la March 23 (M23). Brigedi hiyo inayojulikana kwa kifupi kama FIB, inaongozwa na Mtanzania, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa. Kwa sasa imelidhibiti eneo la Goma.
Edwin Butcher: Hatuhusiani na Dk. Amani
Mmiliki wa duka la nyama linaloitwa Edwin Butcher la Rwamishenye, Bukoba, amejitokeza na kusema kuwa bucha yake haina uhusiano wowote na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, au udini kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
Mapapa wa ‘unga’ watajwa
*Kinondoni, Magomeni, Mbezi, Tanga watia fora
*Wamo Wakenya, Wanigeria, waimba taarab Dar
*Wengine wapata dhamana kimizengwe, watoroka
Vita dhidi ya wauzaji na wasafirishaji dawa za kulevya inazidi kupamba moto, na sasa JAMHURI imepata orodha ya watu wengine 245 wanaotajwa kuwa ndiyo ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu hapa nchini.
Mtendaji mkuu Osha alalamikiwa Tughe
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, amelalamikiwa mbele ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), kuwa anawaongoza kimabavu wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Serikali.
BRN kuinua elimu nchini
Kiwango cha elimu Tanzania kinatarajiwa kupanda, baada ya Serikali kuzindua mpango wa kufanikisha Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN).