Category: Kitaifa
Rushwa yazigonganisha Mahakama, Wizara
Wizara ya Nishati na Madini imeingia kwenye mvutano na Mahakama baada ya mhimili huo kuamuru raia wa China aliyekamatwa akitorosha madini ya tanzanite, arejeshewe madini hayo kinyume cha sheria.
Maswi: Kila Mtanzania atapata umeme
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imesema umeme ni huduma ya lazima kwa Watanzania na itafanya kila liwalo kuhakikisha kila Mtanzania anapata umeme. Msimamo wa Serikali umetolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, wakati akizungumza katika kipindi cha Tuambie kupitia runinga ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wiki iliyopita.
DECI mpya yaibuka Dar
Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali Tanzania kilichopo jijini Dar es Salaam, kimeingia katika kashfa ya kuwatapeli wajasiriamali walioshiriki katika semina za ufugaji kwa kuwapa ahadi hewa.
JWTZ yafyeka majangili
*Operesheni Tokomeza’ yaanza rasmi
*Inashirikisha, Usalama wa Taifa, Polisi
*Majangili kadhaa hatari yakamatwa
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeanza rasmi operesheni ya kuwatokomeza majangili.
Operesheni hiyo iliyopewa jina la Operesheni Tokomeza ilianza rasmi Oktoba 5, mwaka huu ikilenga kuwalinda wanyamapori, hasa ndovu na faru walio hatarini kumalizwa na majangili.
CIDTF: Korosho inaweza kuwainua wakulima
Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga.
Muhongo akagua ujenzi bomba la gesi
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameeleza kuridhishwa kwake na kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.