Category: Kitaifa
Mbowe moto
.Adai moto aliowasha hauzimiki mpaka kieleweke 2015
.Asema anaumizwa kuteketea mamilioni Bunge la Katiba
.Atamba ipo siku polisi watazitambua haki za Watanzania
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema anashangazwa na vigogo wa Jeshi la Polisi kufanya hila za kumkabili, ilhali wanaona namna Watanzania walivyodhulumiwa haki yao kupitia Bunge Maalum la Katiba.
Tanzania yaonywa kuhusu Al-Shabaab
POLISI wa Uganda wameitaka Tanzania kuwa makini na kundi la ugaidi la Al-Shabaab kutoka Somalia, baada ya jeshi hilo kuwakamata watu wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya kigaidi.
Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Kenya kujihami kwa Polisi wao kumuua kwa risasi mtuhumiwa wa ugaidi katika maeneo ya Bondeni mjini Mombasa.
Ni Polisi tena
Siku chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kukutana na wadau wa habari na kuwataka waripoti habari zinazozingatia amani na usalama wa nchi pamoja na kuwafanya raia wawe na imani na jeshi hilo, baadhi ya polisi wamekuwa vinara wa kuendeleza vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa raia, huku mara kwa mara wakitumia nguvu kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Tanzania yaongoza kuvutia uwekezaji
Imeelezwa kuwa Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazovutia uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki. Kadhalika Tanzania inashika nafasi ya tisa barani Afrika.
Pinda hafai kuwa Rais
Ni matumaini yangu kuwa Watanzania wenzangu hamjambo hasa wale Watanganyika walalahoi kama mimi, sizungumzii wale wanaoishi kama wapo paradiso.
Nimesoma magazeti kadhaa, karibu wiki nzima yanazungumzia habari ya ‘mtoto wa mkulima’ Mizengo Pinda eti anataka urais na wengine kuanza kumpigia debe kwamba anafaa eti kwa vile ni muadilifu, pia hana tuhuma za ufisadi.
TMF yatoa ruzuku kwa vyombo vya habari 16
Mfuko wa vyombo vya habari nchini (TMF), kwa mara nyingine, umetoa ruzuku ya Sh. bilion 1.7 kwa vyombo vya habari 16.