JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

Wazanzibari kutibiwa bure

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema serikali hiyo imekusudia kuendelea kutoa matibabu bure kwa wakazi wote wa Unguja na Pemba. Amesema mafanikio hayo yanatokana na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar…

Hujuma korosho

Juhudi za Rais John Magufuli kudhibiti magendo katika biashara ya korosho, maarufu kama ‘kangomba’ zinaelekea kuingia doa kutokana na watendaji aliowaamini katika ngazi ya wilaya kushiriki biashara hiyo, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Taarifa kutoka mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi…

Kilichong’oa mabosi TAKUKURU

Mchezo wa rushwa aliounusa Rais John Magufuli katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ukabila, ukanda na usiri wenye lengo la kunufaisha watu binafsi na jamaa zao, vimetajwa kumsukuma Mkurugenzi Mkuu mpya wa Takukuru, Diwani Athumani, kufumua mtandao…

Apandishwa kizimbani Moshi kwa udanganyifu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, John Bogohe, kwa makosa matatu ikiwamo kutumia nyaraka kwa nia ya kumdanganya mwajiri. Mhasibu huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya…

NSSF watekeleza agizo la Rais

Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli kwa kuhakiki waliokuwa wafanyakazi wa migodi na ajira za muda mfupi.  Akizungumza mwishoni mwa wiki, Meneja Kiongozi wa Matekelezo (Chief Manager Compliance and Data Management), Cosmas…

Siri zavuja Jiji

Siri nzito za mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha mabasi ya kwenda mikoani eneo la Mbezi Luis zimevuja, zikavuruga watendaji na Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, JAMHURI linathibitisha. Baada ya wiki iliyopita gazeti hili kuandika…