JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

Wafuja mamilioni

Ufisadi wa fedha za kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari vilivyobuniwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, ndio uliomfanya Rais John Magufuli, amng’oe kwenye nafasi hiyo, JAMHURI limebaini. Mradi huo ulibuniwa na Luoga kwa kigezo cha kuongeza…

Waliofuja KNCU hawatapona – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali inaendelea na uhakiki wa mali zote za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) na kuonya kuwa hakuna atakayepona kwa wale wote watakaobainika kufuja mali za chama hicho kikongwe nchini. Baadhi ya viongozi…

Wananchi waitunishia Serikali msuli

Mvutano umeibuka kati ya serikali na wakazi wa Kata ya Nyatwari, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara baada ya wananchi hao kutakiwa kuhama huku wao wakipinga amri hiyo. Wananchi hao wametakiwa kuondoka kwenye kata hiyo ili kupisha njia ya wanyama wanaotoka…

Wananchi walilia fidia mradi wa umeme

Wananchi wa maeneo ya Kinyerezi, Chalinze na Tanga waliohamishwa kupisha mradi wa umeme wa North, East, Grid wa (Kv 400), wameilalamikia serikali kwa kushindwa kuwalipa fidia licha ya zoezi la uhakiki wa maeneo hayo kukamilika tangu mwaka 2015. Wakizungumza na Gazeti la…

Serikali yalizwa

Kampuni ya Crown Lapidary ya jijini Arusha inayojihusisha na biashara ya madini imekumbwa na kashfa ya kutorosha madini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 300 (shilingi zaidi ya bilioni 700), JAMHURI limebaini. Madini hayo aina ya Green Garnet, yanatajwa…

Waliofukuzwa kwa ufisadi Bodi ya Kahawa wakimbilia mahakamani

Waliokuwa wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) Makao Makuu mjini Moshi na baadaye kufukuzwa kazi kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 3.4, wameanza kuitunishia misuli serikali. Wafanyakazi hao ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha, Astery Bitegeko…