Category: Uchumi
JAMHURI yaisafisha TTCL
Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imemng’oa katika madaraka Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Said Amir, na kuwasimamisha kazi maofisa wengine watatu waandamizi ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi zinazowakabili.
Wahitimu wa Kibongo wachangamkiwa London
Uzuri wa ng’ombe wa maziwa ni pale akishazaa na kuanza kutoa maziwa kwa wingi. Karibu sawa na hivyo, uzuri wa mwanafunzi machoni pa waajiri ni pale anapohitimu vyema masomo yake na kuwa tayari kwa kazi.
Kashfa mpya Maliasili
[caption id="attachment_73" align="alignleft" width="314"]Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki[/caption]*Kiini macho chaibuka vitalu vya WMA
*Vyatangazwa Kagasheki akiapa Ikulu
*Ni kukamilisha ratiba, matajiri wavinasa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, anakabiliwa na mtihani wa kwanza ndani ya wizara hiyo, baada ya kuibuka kwa kashfa mpya katika ugawaji vitalu 13 vya uwindaji vinavyomilikiwa na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs).
Vitalu hivyo ni tofauti na vile vilivyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Ezekiel Maige. Habari za uhakika kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na katika WMA, zinaonyesha kuwa kutangazwa kwa vitalu hivyo kumefanywa haraka haraka siku Kagasheni na mawaziri wenzake walipokuwa Ikulu wakiapishwa.
TANESCO yapata mafanikio nchini
*Yafikishia umeme Watanzania asilimia 18.4, mita 65,000 za Luku zaingia
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limeanza kupiga hatua kutokana na juhudi linazofanya za kuwafikishia umeme Watanzania walio wengi.
Waandamanaji kupinga unyonyaji wa Barrick
Mkutano wa mwaka huu wa Barrick Gold Mine uliofanyika Toronto, Canada, umeingia dosari ya maandamano.
EWURA yazidi kubana wachakachuaji
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mafuta na Maji (EWURA) sasa imepiga hatua nyingine na kufanikiwa kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ya dizeli na petroli, baada ya kuanza kutumia teknolojia ya vinasaba (maker).