JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Uchumi

Walarushwa hawa hapa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imetangaza hadharani washitakiwa wote waliopatikana na hatia katika kesi zinazohusu rushwa.  Taarifa ya ambayo gazeti hili imeipata inasema kutajwa kwa washitakiwa hao ni utaratibu mpya unaoanza kutumika mwezi huu, ikiwa ni…

Nauli za daladala kushuka Machi 18

Nauli za daladala nchini zinatarajia kushuka mwishoni mwa mwezi huu kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta nchini na duniani kwa ujumla.   Mwenyekiti  wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DRCOBOA), Sabri Mabrouk, ameiambia JAMHURI…

Bandari Dar inakufa

*Mkurugenzi Mkuu Kipande aingiza ukabila, udini, majungu

*Wafanyakazi watatu bandarini wafariki kutokana na vitisho

*CCTV hazifanyi kazi tangu 2011, wachonga dola mil. 6.5

*Mnikulu Gurumo, Mtawa wampa kiburi, wachafua jina la JK

*Amdanganya Dk. Mwakyembe, amtukana Balozi wa Japan

Kuna kila dalili kuwa Bandari ya Dar es Salaam inakufa kutokana na uongozi mbovu uliojiingiza katika majungu, udini, ukabila na majivuno yasiyo na tija. Wafanyakazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamepoteza morali wa kufanya kazi kutokana na vitisho na matusi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Madeni Juma Kipande.

Hadi habari hii ya kiuchunguzi inachapishwa wafanayakazi watatu; Peter Gwamaka Kitangalala, Dotto Mbega na mwingine aliyefahamika kwa jina la Lyochi wamefariki dunia katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na shinikizo la damu lililozaa kiharusi baada ya vitisho vya Kipande.

Katika hali ya kuwavuruga wafanyakazi wa bandari, Katangalala alihamishiwa Mwanza na baada ya miezi miwili akahamishwa tena kwenda Lindi, huku akipewa vitisho kuwa muda wowote ajiandae kufukuzwa kazi. Kutokana na hofu, alipata kiharusi (stroke) akafa. Mbega kwa upande wake yeye alikuwa makao makuu Dar es Salaam, lakini kutokana na vitisho vya kila siku vya Kipande na wasaidizi wake, naye akapata kiharusi mwezi mmoja uliopita akafariki dunia.

Jumapili ya Machi 30, mfanyakazi mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Lyochi huku wengine wakisema ni Oluwochi mwenye asili ya Wajaruo, aliyehamishiwa bandari ya Kasanga, Sumbawanga naye aliaga dunia kwa ugonjwa huo huo wa kiharusi kutokana na mashinikizo ya Kipande.

“Uhalisia hali inatisha. Kipande anajinadi kuwa atamfukuza kila mtu, na kweli anafukuza anaajiri watu wa dini yake. Kuna kabila la Wahaya kutoka Kanda ya Ziwa, hilo utadhani waliwahi kushikana nalo ugoni. Mhaya yeyote aliyemkuta kazini ameapa kumg’oa. Amehamisha [Hassan M.] Kyomile kwa sababu ya kabila lake na kwamba aliomba kazi ya Ukurugenzi Mkuu,” kilisema chanzo chetu.

Kyomile amehamishwa Machi mwaka huu, kutoka makao makuu alikokuwa Mkurugenzi wa Ununuzi na kwenda kuwa Meneja wa Bandari Tanga.

Mwalimu amtia mimba mwanafunzi

Mwalimu Nelson Bashulula anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya kutwa ya Rubale iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, anatuhumiwa kwa kosa la kumtia mimba mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo (jina linahifadhiwa).

Maswi: Kila Mtanzania atapata umeme

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imesema umeme ni huduma ya lazima kwa Watanzania na itafanya kila liwalo kuhakikisha kila Mtanzania anapata umeme. Msimamo wa Serikali umetolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, wakati akizungumza katika kipindi cha Tuambie kupitia runinga ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wiki iliyopita.

Muhongo akagua ujenzi bomba la gesi

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameeleza kuridhishwa kwake na kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.