Category: Siasa
TCRA yakamilisha anwani za makazi
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekamilisha mpango wa kuwapatia Watanzania anwani za makazi.
Membe amkamata Kitine pabaya
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, ameshindwa kumtaja waziri anayedai kwamba amechota fedha katika mataifa kadhaa kwa ajili ya kujenga hoteli na kujiandaa kugombea urais mwaka 2015.
Dk. Kitine alipokuwa akihojiwa katika Kituo cha Televisheni cha Channel 10 cha jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alidai kwamba waziri huyo ana kiasi kikubwa cha fedha.
Zitto atoa ya moyoni
[caption id="attachment_62" align="alignleft" width="133"]Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe[/caption]Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, mwishoni mwa wiki amefanya mahojiano maalum na Gazeti la JAMHURI kuhusiana na mwenendo wa Bunge na mwelekeo wa taifa hili kwa ujumla. Mwandishi Wetu DEODATUS BALILE anakuletea mahojiano hayo kama ifuatavyo:
Vigogo watafuna nchi
*Wabunge wawili CCM walipwa fidia Sh milioni 964 bado jengo lauzwa
*Zitto asema kalinunua Fida Hussein
*Ataka Katibu Mkuu Fedha ahojiwe
Wakati Rais Jakaya Kikwete amebadili Baraza la Mawaziri kutokana na shinikizo la Bunge, taarifa zimevuja kutoka serikalini kuwa kuna vigogo na watendaji wakuu wanaouza mali za umma kama zao.
Orodha vigogo waliokalia kuti kavu yaanza kuvuja
[caption id="attachment_58" align="alignleft" width="139"]Rais Jakaya Kikwete[/caption]Ikulu imeanza kuorodhesha watumishi wa umma wanaopaswa kufukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka, kutokana na kuhusishwa na ufujaji fedha za umma kama ulivyoainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Takukuru inajipendekeza kwa Rais Kikwete?
“Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu (ili) tuanze kuyashughulikia haraka,” anasema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah.