Category: Siasa
Bila kumpata Kagame wetu tutakwama
Nilipata kusoma makala ya kiongozi wangu wa kitaaluma, Jenerali Ulimwengu, akikosoa Watanzania wenye matamanio ya kumpata ‘Kagame’ wao.
Mzimu uliowanyoa mawaziri unahitaji tambiko—2
Wiki iliyopita nilibainisha kuwa kiini cha tatizo la ufisadi wa nchi hii inaonekana hakijabainika; ndiyo maana tunahangaika na matokeo badala ya kiini.
Mabomu Mbagala siri zavuja
*Wakubwa walitumia (msiba huo) kutengeneza utajiri binafsi
*Ofisi ya Pinda yahaha kutafuta zaidi ya bilioni fidia mpya
*Waliopunjwa kucheka, hundi hewa milioni 260 zadoda
Miaka mitatu baada ya mabomu kulipuka katika Kambi ya Jeshi Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, siri nzito zimeanza kuvuja jinsi wakubwa walivyotumia msiba huo kujitengenezea utajiri binafsi.
Napata wasiwasi kuhusu upotoshaji huu
Nimesoma makala katika gazeti moja litolewalo kila siku, yenye kichwa cha habari, “NIDA imemdhalilisha Rais, majeshi iombe radhi”. Katika makala hayo, mwandishi amejitahidi kuueleza umma kile anachoamini ni ukweli, wa taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari nchini na baadaye kuja kufafanuliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuhusu sakata la vyeti 948 vya majeshi yetu kuwa feki (kughushi).
NIDA waungwe mkono wanafanya kazi muhimu
[caption id="attachment_80" align="alignleft" width="160"]Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu[/caption]Vitambulisho vya taifa ni kitu muhimu sana katika ustawi na maendeleo ya taifa letu. Kukamilishwa kwa mchakato wa vitambulisho vya taifa kwa Watanzania na wageni mbalimbali hapa nchini, ni juhudi na mafanikio makubwa ya Serikali na watumishi waliojitoa kwa nguvu na maarifa yao yote kufanikisha azma hii.
TCRA yakamilisha anwani za makazi
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekamilisha mpango wa kuwapatia Watanzania anwani za makazi.