JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Ufisadi watikisa Bunge

*Unahusu kada wa CCM anayechimba urani

*Profesa Tibaijuka amtwika mzigo Jaji Werema

*Naibu Spika aagiza Waziri Muhongo ajiandae

*Sinema nzima imeibuliwa na Halima Mdee

 

Wafanyabiashara ndugu wanaodaiwa kubadili matumizi ya ardhi kutoka uwindaji wa kitalii na kuanza harakati za uchimbaji madini ya urani, wameibua mgongano mkubwa bungeni na serikalini. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amemwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, asaidie kupata utatuzi kashfa hiyo.

Hotuba ya Lissu iliyolitikisa Bunge, Serikali

*Atoboa siri majaji wengi ‘vihiyo’, washindwa kuandika hukumu

*Aeleza namna wakuu wa wilaya walivyoteuliwa kwa rushwa

*Yumo mwingine aliyehukumiwa kwa ubaguzi wa ukabila

Ifuatayo ni sehemu ya maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kuhusu Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013. Lissu alitoa maoni haya na kwa kiasi fulani yaliibua mjadala mkali bungeni, huku Serikali ikitaka aondoe baadhi ya maneno, na yeye akakataa. Endelea…

UTEUZI WA MAJAJI

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua ukweli kwamba Rais Kikwete ameteua majaji wengi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kuliko marais wengine wote waliomtangulia kwa ujumla wao. Rekodi hii peke yake inaonyesha kwamba Rais anatambua umuhimu wa Mahakama Kuu kuwa na watendaji wa kutosha wa utoaji haki ili kutekeleza dira ya ‘haki kwa wote na kwa wakati.’

‘Majaji ndiyo waliomtuma Lissu’

Hotuba kali ya Tundu Lissu ya kukosoa uteuzi wa majaji dhaifu uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, imeelezwa kwamba ina baraka zote za baadhi ya viongozi waandamizi wa Mhimili wa Mahakama, JAMHURI limeelezwa.

HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

 

DIRA YA WIZARA:

Kuwa na uhakika wa milki za ardhi, nyumba bora na makazi endelevu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

 

DHIMA:

Kuweka mazingira yanayofaa kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma za ardhi, nyumba na makazi

 

Wapinzani wachekelea Pinda kugwaya

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kufarijika na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba kampuni ya Agrisol haijapewa ardhi ya Katumba na Mishamo mkoani Katavi.