JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Mkakati wa 2015 waiva

Makundi ya kuhasimiana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yameendelea kukiburuza chama hicho kwa kuimarisha mkakati wa kupachika wagombea wao kwenye nafasi mbalimbali ikiwamo Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC-CCM).

Kituo cha yatima chadaiwa kugeuzwa biashara

 

Katika kipindi hiki cha mageuzi ya kijamii, kumekuwa na mashirika mbalimbali yaliyoanzishwa nchini yakijitanabaisha kuwa yanalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, kwa mashirika hayo kuwapatia watoto hao mahitaji muhimu kama vile chakula, malazi, mavazi, matibabu na elimu.

Matajiri wahujumu kilimo nchini

Wakati Tanzania ikipambana kujiondoa katika adha ya njaa kwa kuboresha kilimo nchini kupitia mradi wa Kilimo Kwanza, wafanyabiashara wenye uchu wa utajiri wa haraka wanahujumu kilimo. Matajiri hawa wanapewa fedha za ruzuku kusambaza mbolea, lakini wanafanya kufuru. Kinachotokea, badala ya kuwapelekea wakulima mbolea, wanawapelekea mbolea iliyochanganywa saruji, chumvi na mchanga.

Fedha za rushwa Hanang’ zatisha

 

 

 

Vita ya kuwania nafasi ya NEC kupitia Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara, imechukua sura mpya baada ya mmoja wa wagombea wanaoelezwa kuenguliwa kwenye Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Hanang’ kubuni mbinu mpya za kampeni.

 

Mzungu aiweka Serikali mfukoni

Raia anayesadikiwa wa Ubelgiji anayetafutwa na Serikali kwa ukwepaji kodi wa zaidi ya Sh bilioni 10, Marc Rene Roelandts, analindwa na baadhi ya watumishi na viongozi wa Serikali, JAMHURI imeelezwa. Kwa sasa mfanyabiashara huyo yuko mafichoni nje ya nchi kutokana na tuhuma zinazomkabili, lakini habari zinasema watumishi wake wawili wamekamatwa.

Kagasheki afyeka Kamati ya Vitalu

*Awatupa Jaji Ihema, Beno Malisa, Daniel Nsanzugwanko

*Pia wamo Mbunge Mwanjelwa, Kijazi, Profesa Rutashobya

*Chanzo ni tuhuma za rushwa ugawaji vitalu vya uwindaji

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ameifuta kazi Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii. Kamati hiyo, pamoja na mambo mengine, imelalamikiwa mno kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wajumbe wake zaidi ya 10.