JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

TRA: ETR itaboresha biashara, mapato ya Serikali

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua Awamu ya Pili ya utekelezaji wa Mfumo wa Mashine za Kielektroniki (ETR), kwa wafanyabiashara  zaidi ya 200,000 wenye mauzo ghafi ya Sh milioni 14 kwa mwaka.

Lipumba, Limbu wamponda Spika

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema staha ya Bunge itazidi kuporomoka ikiwa utaratibu wa kumtumia Spika anayetokana na chama cha siasa hautabadilishwa.

Kashfa yamkumba Naibu Spika Ndugai

*Mwanamke ‘mgeni wake’ adaiwa kumpoka maelfu ya dola kitaalamu

*Yeye amgeuzia kibao mtumishi wa ndani, amsweka rumande siku saba

*Mtumishi wa ndani afukuzwa, aieleza JAMHURI kila kilichotokea

*Walinzi wawili wa kike wasimamishwa, mishahara, posho vyafyekwa

 

Kuna harufu ya kashfa dhidi ya Naibu Spika, Job Ndugai, ambaye ameibiwa dola 15,000 (Shilingi zaidi ya milioni 24), nyumbani kwake Area ‘D’ mjini Dodoma.

Takataka za serikali katika Elimu

 

*Dk. Kawambwa aliamua, sasa anamrushia mzigo Dk. Ndalichako

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao cha magwiji 14 wa elimu kilichobariki utaratibu mpya wa matumizi ya viwango vya ufaulu katika Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, uamuzi ulibadilika na kuonekana kama takataka katika jamii.

Dini kuondoa upotoshaji wa kuchinja wanyama

Viongozi wa dini nchini wamekubalina kutoa tafsiri ya kuchinja kwa waumini wao, kuondoa upotoshaji na kurejesha uelewano baina yao.

‘Watanzania tembeleeni hifadhi za taifa’

Watanzania wamehimizwa kujenga mazoea ya kutembelea Hifadhi za Taifa, kujionea vivutio vilivyopo na kujifunza mambo mbalimbali badala ya kusukuma jukumu hilo kwa wageni kutoka nchi za nje pekee.