JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Ndugu wa Barlow wataka IGP Mwema awajibu

Ndugu wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow aliyeuawa kwa kupigwa risasi, wamesema wanataka majibu ya kina kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema.

JWTZ: Hizi ni rasharasha

*Wasubiri wenzao A. Kusini, Malawi zianze za masika

*Kamanda: Matumaini ya Wakongo ni makubwa mno

*Waziri wa Ulinzi asema hali za vijana nzuri

Brigedi ya Jeshi la Umoja wa Mataifa (UN) la Kulinda Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) inayoongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ipo salama na inajiandaa usiku na mchana kuhakikisha amani inarejeshwa katika eneo hilo.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba operesheni rasmi inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu baada ya vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi, kuungana na wenzao wa JWTZ ambao tayari wapo eneo hilo.

 

JWTZ: Hizi ni rasharasha

*Wasubiri wenzao A. Kusini, Malawi zianze za masika
*Kamanda: Matumaini ya Wakongo ni makubwa mno
*Waziri wa Ulinzi asema hali za vijana nzuri Brigedi ya Jeshi la Umoja wa Mataifa (UN) la Kulinda Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) inayoongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ipo salama na inajiandaa usiku na mchana kuhakikisha amani inarejeshwa katika eneo hilo. Habari za uhakika zinaeleza kwamba operesheni rasmi inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu baada ya vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi, kuungana na wenzao wa JWTZ ambao tayari wapo eneo hilo. 

Jeshi la ‘bodaboda’ latembeza mkong’oto wilayani Geita

Jeshi lisilo rasmi la vijana zaidi ya 60 wanaofanya kazi ya kubeba abiria kwa kutumia pikipiki (bodaboda), huku wakiimba kibwagizo cha ‘wapigwe tu’, wameteka mtaa na kutembeza kipigo kikali kwa abiria wao mmoja.

MAUAJI YA BARLOW

 

Malele aendelea kuteseka Muhimbili

Maendeleo ya matibabu ya Mohamed Malele aliyetangaza siri za mtandao unaodaiwa kuhusika kumuua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, ni kitendawili.

MAPAMBANO NA WAASI DRC

JWTZ yaifumua M23

*Wachakazwa kwa saa mbili, wakimbia waacha silaha, vyakula

*Yaelezwa wapo msituni wanashindia matunda kama ngedere

Majeshi ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) yanayoongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yameanza kupata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya waasi.