Category: Siasa
Hotuba ya Lissu iliyosababisha TBC1 ‘izimwe’
Aprili 12, mwaka huu, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu aliwasilisha maoni ya Wajumbe walio wachache katika Kamati Namba Nne kuhusu sura ya kwanza nay a sura ya sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati akiwasilisha, Televisheni ya Taifa (TBC1) ilikata matangazo yake katika kile kilichotafsiriwa na wengi kuwa ni kuuepusha umma kupata maoni ‘makali’ yaliyomo kwenye hotuba ya Lissu. Kwa kuzingatia haki ya wananchi ya kupata habari, JAMHURI inawaletea hotuba hiyo neno kwa neno. Endelea
UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’) ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa suala la muundo wa Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya Sita inahusu ‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya miaka thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya chama hicho imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi.”
Suala hili pia limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka mitatu iliyopita. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba wakati wa kuwasilisha Ripoti ya Tume yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar tarehe 30 Disemba, 2013: “Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu Rasimu ya awali ilipotolewa … ni Muungano wa Tanzania. Jambo kubwa limekuwa juu ya muundo wa Muungano.”
Umuhimu wa suala hili unathibitishwa pia na uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum kuelekeza kwamba Kamati zake Namba Moja hadi Kumi na Mbili zianze kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Haya ni maoni ya wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne juu ya Sura hizi mbili.
Wakubwa wanavyotafuna Bandari
Majambazi wajitangazia Serikali
*Wajiundia Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo
*Wabuni bendera, mahakama na polisi yao
*Vijiji vyawatii, waendesha ujangili, ujambazi
Watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na majangili, wamejiundia serikali ndani ya Msitu wa Igombe mkoani Tabora, JAMHURI inathibitisha.
Wamejiundia uongozi madhubuti pamoja na jeshi walilolipa jina la Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa huenda idadi ya watu hao ikawa kubwa kuliko inavyodhaniwa, kwani wanadaiwa kusambaa ndani ya misitu minene katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Pia wapo katika maeneo kadhaa ya Mkoa wa Kigoma.
Imebainika kuwa watu hao wapo katika Msitu wa Igombe uliopo wilayani Uyui na kusambaa katika mapori mengine ya Malagarasi na Myowosi; na walianza kujiimarisha tangu mwaka 2010.
Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanaounda ‘serikali’ hiyo wanatoka katika makabila kadhaa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga, Arusha, Kigoma na katika mataifa jirani, hasa Burundi.
“Serikali” hiyo batili ina jeshi lake la ulinzi, jeshi la polisi, mahakama na vyombo vingine vya utawala.
Shughuli kuu zinazofanywa ni ujambazi, ujangili, kilimo cha bangi, biashara ya mbao, uuzaji bunduki pamoja na risasi; na uhalifu wa aina nyingine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, amezungumza na JAMHURI na kusema, “Ni kweli tuna tatizo hilo. Lipo na ni kubwa. Serikali imeshalitambua, na hatua zinachukuliwa.”
Mwasa, licha ya kukiri, hakutaka kuingia kwenye undani wa suala hilo katika kile kinachoonekana kuwa ni kutotaka kutibua hatua za kiusalama zilizopangwa kuchukuliwa na vyombo vya dola katika kukabiliana na genge hilo.
Hata hivyo, maneno ya Mwasa katika kuthibitisha ukubwa wa jambo hili ni haya, “Kweli tatizo lipo…ni kubwa kuliko unavyofikiri.”
Watu wawili waliokamatwa na baadaye kutoroka kutoka mikononi mwa kundi hilo wamesema genge hilo ni masalia ya wale walioshughulikiwa na Serikali mwaka 2010. Majina ya watu hao tunayahifadhi kutokana na sababu za usalama wao.
“Kuna jeshi lenye askari wa jadi wenye bunduki za SMG (Sub Machine Gun), na magobore. Wanaendesha uasi. Wamepandisha bendera ya bluu, imeandikwa Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo. Wahalifu wengi wageni wanatoka Burundi. Wanashirikiana na Wasonjo, Wasukuma na Waha.
“Shughuli zao ni kilimo cha bangi, kupasua misitu, uwindaji haramu na n.k. Wana watemi wao. Kila mtemi analindwa na askari wasiopungua 20,” anasema mmoja wa watoa habari wetu.
Uimara wa magenge hayo ya wahalifu yaliyojiimarisha yamewafanya hata wananchi na viongozi wa vijiji jirani na mapori wanamoishi, wawe watiifu kwao.
“Ukiwa na tatizo unaenda msituni kuomba msaada wa askari kukukamatia mhalifu au mbaya wako. Wanatumwa askari wanakuja kukuteka na kukupeleka huko msituni.
Nyalandu ‘auza’ Hifadhi
*Yeye, James Lembeli waenda Afrika Kusini kukamilisha mpango
*Baada ya Katavi Hifadhi nyingine nazo zitatolewa kwa wawekezaji
*Katibu Mkuu ashinikizwa, abaki njia panda kuidhinisha safari, malipo
*Urafiki wa Waziri, Lembeli waibua shaka miongoni mwa watumishi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, yupo kwenye hatua za mwisho za kuikabidhi Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa mwekezaji wa Afrika Kusini.
Bilionea Lake Oil kitanzini
*Yeye, wenzake wafungiwa vituo kwa kuchakachua *Walipa mamilioni ya shilingi Kampuni ya Lake Oil inayomilikuwa na bilionea Ally Awadh, imeingia matatani baada ya vituo vyake vinne vya mafuta kufungiwa kutokana na kuuza mafuta yasiyokuwa na vinasaba. Vituo vilivyofungwa ni Lake…
Ufisadi wa kutisha Mamlaka ya Ngorongoro
*Mapato ya Sh milioni 300 yaingia mifukoni *Safari hewa zagharimu shilingi bilioni 1.316 *Bia, soda, teksi vyagharimu Sh milioni 133 *Masurufu pekee yalamba shilingi milioni 100 Ufisadi wa kutisha umebainika kuwapo katika Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA), huku Serikali…
- TMA yatoa matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano
- Mtoto aliyetekwa anasuliwa kwa mtekaji akiwa hai na afya njema
- Rais Dkt. Samia azindua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro
- Rais Samia : Tanzania ni msimamizi Mpango wa Nishati Safi Afrika
- TAWA na Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Morogoro
Habari mpya
- TMA yatoa matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano
- Mtoto aliyetekwa anasuliwa kwa mtekaji akiwa hai na afya njema
- Rais Dkt. Samia azindua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro
- Rais Samia : Tanzania ni msimamizi Mpango wa Nishati Safi Afrika
- TAWA na Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Morogoro
- RC Mtaka: Rais Samia ameibeba sekta ya kilimo mabegani mwake katika miaka 4 ya uongozi wake
- Rais Mwinyi : Mradi wa EACOP ni kioo cha maendeleo ya sekta ya mafuta Afrika Mashariki
- Mashambulizi ya Urusi yaua watu 25 Ukraine
- Rais Samia : Serikali ina dhamira ya kujenga Tanzania jumuishi yenye ustawi wa haki na kupinga ubaguzi
- Rais Samia: Tanzania imetekeleza malengo 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s)
- Rais Samia akihutubia wananchi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
- Maandamano ya wanawake kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
- Rais Dk Samia akiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
- Matukio mbalimbali kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
- Akamatwa kwa kung’oa bendera za CUF Kondoa