JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

M23 walia njaa

Waona giza nene mbele yao, Uganda yaonya vita inanukia
DRC yazidisha mashaka kwa Uganda, Watanzania waonya

Hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kukataa kusaini mkataba wa amani na kundi la waasi la M23, imepeleka kilio kwa kundi hilo, na sasa wanalia njaa uhamishoni nchini Uganda.

Wastaafu  wahoji hati ya Muungano Pemba, Unguja

Wastaafu wa kada mbalimbali serikalini wameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) chini ya  Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, kuonesha hati ya  Mungano wa Unguja na Pemba iwapo visiwa hivyo viliungana kisheria na mkataba kutambuliwa na Umoja wa Mataifa.

ADC: Dk. Shein anamuogopa Maalim Seif

Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema kitendo cha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kutomchukulia hatua za  kisheria Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, kutokana na  ofisi yake kutumia vibaya fedha za umma kinyume cha sheria, kimeupaka matope utawala wake na huenda anamuogopa kiongozi huyo.

Hukumu yamliza bibi kizee

Hukumu ya kesi ya rufani namba 285/2012 iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa Mkoa wa Mwanza, imemliza Bibi Kizee, Moshi Juma  Nzungu (67), kwa hofu ya kunyang’anywa nyumba anayoishi tangu miaka ya 1957 katika eneo la Pasiansi, jijini Mwanza.

Katiba haiandikiki

  • CCM, Chadema, Profesa Shivji wasema muda hautoshi
  • Jaji Mtungi aonya, mnyukano waendelea, hofu yatanda

Kuna kila dalili kuwa Katiba mpya iliyotarajiwa kuzinduliwa Aprili 26, 2014 haiandikiki kwa maana kuwa muda huo hauwezi kutosha kukamilisha mchakato wa kupata Katiba hiyo, vyanzo vimelieleza gazeti la JAMHURI.

Magufuli amvimbia Pinda

Kuna kila dalili kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli, amekataa au kushindwa kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na kilichoelezwa kuwa kuyatekeleza ni kuvunja sheria ya usalama barabarani na kanuni zake, hivyo yeye hayuko tayari kufanya hivyo.