JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Mjane Geita aelezea Finca ilivyompora mali

Yakomba majokofu mawili, televisheni, deki

Pia jenereta kubwa kwa deni la Sh. 600,000

Mama aona maisha magumu, ataka kujiua

 

Malalamiko dhidi ya Benki ya FINCA Tanzania, Tawi la Geita, kwamba inanyanyasa wajasiriamali, yamemuibua mjane aliyeeleza alivyoporwa kwa mabavu vitu vyake vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 1.65 kabla ya kuuzwa kwa bei ya Sh 600,000.

Waziri afagilia ‘JAMHURI’ wa akisimamia bomoabomoa

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene, Alhamisi iliyopita alishindwa kuzuia hisia zake, pale alipolipa sifa Gazeti la JAMHURI huku akisimamia ubomoaji wa mgahawa uliojengwa katika eneo la wazi jijini.

Sadifa atangaza vita dhidi ya Maalim Seif

 

.Amtuhumu kuwa ni kibaraka wa Waarabu

.Adai Seif akipewa nchi, ataiuza asubuhi

.Rais Dk. Shein amsifu Sadifa hadharani

.CUF waijia juu Polisi, wadai Sadifa ni…

 

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Khamis Sadifa Juma, ametangaza hadharani vita ya kupambana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad.

Lowassa amtesa JK

Waanza zengwe la tatu bora
Kinana akata mzizi wa fitina

 

 

Taarifa kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, huenda akaenguliwa iwapo atatangaza nia na kuchukua fomu kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimezidi kushika kasi.

China kuboresha Makumbusho ya Mwalimu Nyerere

Kwao neno la kwanza kujifunza ni ‘rafiki’ jina la kwanza wanalojua ni ‘Nyerere’

 

Kwa baadhi ya Watanzania, jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, si muhimu sana kwao. Hii pengine inathibitisha ule usemi wa ‘nabii hakubaliki kwao’.

liyepooza miguu, kutimuliwa Bugando apona kwa mganga

Miezi michache baada ya baadhi ya madaktari na wauguzi wa Hospitali Teule ya Bugando kumtimua mgonjwa aliyeoza makalio akiwa wodini, kijana mwingine aliyepooza mwili kuanzia kiunoni hadi miguuni naye ameondolewa.