JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Kumekucha urais

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; imedaiwa kuwa anaendesha kampeni kali ‘kimyakimya’ kuhakikisha anateuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania kiti cha urais mwaka huu. Habari za kiuchunguzi zisizotiliwa shaka ilizozipata Gazeti la JAMHURI, zinaonesha…

Kiwanda cha Sukari chafutwa uwekezaji

Wimbi la uingizwaji wa sukari nchini kwa njia ya magendo limeleta athari kubwa kwa viwanda vya ndani na baadhi yao sasa vimeanza kupunguza wafanyakazi pamoja kufuta baadhi ya mipango yake ya uwekezaji ya muda mrefu.

Warembo wa India, Nepal watumikishwa ngono Dar

. Uhamiaji yawanasa Mwananyamala Kisiwani

. Yawaokoa, wasimulia mateso makali ya jijini

. Walikuwa ni watu wa klabu tu, hawalijui jua

. Waliambiwa hapo Mwananyamala ni ‘Sauzi’

. Warejeshwa kwao, waliowaleta waadhibiwa

. Sasa waziponza klabu za Continental, Hunters

. Raha ndani ya klabu hizo sasa ‘zaota mbawa’

 

Kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa mwaka jana (2014), wasichana 22 kutoka nchi za Nepal na India, walitumikishwa ngono na kufanyiwa vitendo vya kinyume na haki za binadamu.

Bosi NIC ang’olewa

* Bodi yakatisha mkataba ghafla

* Afika ofisini akuta kufuli mlangoni

* Mwenyewe adai umri wa kustaafu

Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Justine Peter Mwandu, sasa ameondolewa kazini akiwa amebakiza mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja wa utumishi wake, imefahamika jijini Dar es Salaam.

Mwekezaji ahusishwa kifo Katibu wa Chadema

Watu watatu akiwamo Polisi Jamii wa Kijiji cha Ming’enyi, Kata ya Gehandu, Hanang mkoani Manyara, wanadaiwa kumuua Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tawi la Kijiji, Andu Kero.

Lissu amuonya Chenge

*Asema mchezo wa kutumia mahakama haumsaidii

*Amdonoa Rais JK, awatahadarisha wasaidizi wake

*Ataka Jaji Werema afikishwe mahakamani haraka

*CCM yawatosa rasmi Chenge, Prof. Tibaijuka, Ngeleja

 

 

Mwanasheria Mkuu wa chama kikuu cha upinza – Chama cha Maendeleo na Demokrasi (CHADEMA), Tundu Lissu amesema Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Andrew Chenge anachokifanya mbele ya macho ya Watanzania kwa sasa ni kukwepa kujieleza hadharani.