JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Makanisa mengi ni dalili ya kukata tamaa

Juzi nimesoma habari inayohusu utajiri wa kutisha, wa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya kikristo. Viongozi wanaotajwa, wengi wao ni hawa wa madhehebu yanayoibuka na kusajiliwa kila siku. Nilifurahi kusoma habari hiyo kwa sababu imebeba kile ambacho mara zote nimekiamini.

Yanga ina jinamizi la saikolojia

Kila upande wa mabingwa wa kandanda Afrika Mashariki na Kati, Dar es Salaam Young Africans (Yanga) yenye makao yake makuu katika mitaa ya Jangwani na Twiga jijini, unaelekea kukabiliwa na jinamizi la kisaikolojia.

Zijue amri 10 za kujihakikishia umasikini milele

Mpendwa msomaji, najua juma lililopita vyombo vya habari vilitawaliwa na mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi. Nawashukuru wanahabari kwa mshikamano waliouonesha nchi nzima kwa maandamano, wanahabari tuendelee hivi hivi bila kutetereka.

Tanzania nako kuna 
Okwi, Bocco, Bahanuzi

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inayodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, hatimaye imeanza Jumamosi iliyopita huku timu tatu za Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club mabingwa watetezi, Azam (Wanalambalamba) iliyoshika nafasi ya pili na Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ya mitaa ya Jangwani na Twiga, zote za jijini zikipewa nafasi kubwa ya kuitawala.

Falcao kumchachafya Ronaldo?

Msimu uliopita, mshambuliaji wa Atletico Madrid, Falcao, alifunga mabao 23 katika Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), hatua iliyomfanya awe wa tatu nyuma ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, lakini wote wakiongozwa na mwanasoka bora wa dunia anayeichezea Barcelona, Lionel Messi.

Rais Kikwete tuokoe Karagwe, Runyogote anatumaliza

Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete, Salaam. Mei 30, 2012, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, walimwandikia Mkurugenzi Mtendaji barua wakimtaka aitishe kikao maalumu cha Baraza la Madiwani, kujadili tuhuma mbalimbali za ufisadi walizozielekeza kwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Kashunju Runyogote.