Category: MCHANGANYIKO
Nashukuru, utabiri kwa Nyalandu unatimia
Tangu mapema kabisa nilishasema kwamba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ni tatizo. Niliyasema haya wiki kadhaa baada ya kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.Nyalandu alianza matatizo tangu akiwa Wizara ya Viwanda na Biashara. Nadhani Dk. Cyril Chami, anaweza kuwa msaada mzuri katika hili ninalolisema.
Uhuru umeyeyusha matarajio yetu
Desemba 9, mwaka huu, Watanzania tumeadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa nchi yetu, huku wengi wetu wakikabiliwa na maisha magumu kupindukia. Binafsi ninaamini kuwa ni unafiki kusema Tanzania haina cha kujivunia, lakini pia ni unafiki kusema Serikali kupitia Uhuru huu, imeboresha maisha ya wananchi.
Mihadarati sasa yapigiwa upatu
Nilipokuwa nchini Ghana kwa mafunzo ya vitendo mwishoni mwa miaka ya ’80, nilishangazwa na daktari mmoja. Nakumbuka ilikuwa katika Korle-Bu Teaching Hospital ya Chuo Kikuu cha Accra, na bado sijausahau mtaa wake – Guggisberg Avenue katika mji mkuu, Accra.
Yah: Kama ningekuwa Waziri wa Usalama Barabarani
Wanangu, nawapa kongole ya kutimiza miaka 51 ya Uhuru mlionao hivi leo, nawapongeza kwa kuwa sisi wana-TANU ni kama ndoto ya kuamini kuwa tumeweza kuhimili vishindo vya wakoloni kwa kipindi chote hiki.
Sarafu moja Afrika Mashariki ni mtego
Wiki iliyopita hapa nchini umekuwapo mjadala wa kiuchumi, unaohoji mpango wa kuharakisha matumizi ya sarafu moja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mjadala huu umehusisha wadau mbalimbali, akiwamo Balozi wa Tanzania nchini Ubeligji, Dk. Diodorus Kamala.
DC Geita ageuka kituko
Mkuu wa Wilaya (DC) ya Geita, Manzie Mangochie, ameingia kwenye vita ya maneno na waandishi wa habari wilayani humo. Katika hatua ambayo haijapata kutekelezwa na DC yeyote, sasa Mangochie, anataka taarifa za waandishi wote, pamoja na sifa zao za elimu. Hoja yake ni kwamba anataka kuandaa “Press Cards”; jambo ambalo kwa miaka yote limekuwa likifanywa na Idara ya Habari (Maelezo).