Category: MCHANGANYIKO
Taifa limefikishwa mahali pabaya
Nguvu na Mamlaka ya Umma ni maneno matano yanayobeba dhana pana ya falsafa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA. Kwa wale ambao kwa bahati mbaya au hata kwa makusudi ni wavivu wa kufikiri, wazo au hata matumizi ya misuli siyo maana wala lengo la falsafa hiyo.
RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
Jumatano Februari 27, 2013 Coastal Union Vs Ruvu Shooting Yanga SC Vs Kagera Sugar Polisi Moro Vs Mgambo JKT JKT Ruvu Vs Totot Africans Mtibwa Sugar Vs TZ Prisons
Malinzi: Tuelekeze nguvu Morocco vs Taifa Stars
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera, Jamal Malinzi, amewataka Watanzania kuiunga mkono Taifa Stars iweze kushinda katika mchezo kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia unaotarajiwa kufanyika Machi 24, mwaka huu.
Yah: Yawezekana maendeleo au tumelogwa?
Siamini kama mtu ambaye anayemwamini Mwenyezi Mungu anaweza kuamua, kwa mkono wake, kukatisha maisha ya mtumishi wa bwana kwa moyo safi na wa kijasiri. Haya naona ni maendeleo mengine ambayo enzi zetu hayakuwako, sielewi kama napaswa kuwapongeza au kuwalaumu kwa maendeleo hayo.
fasihi fasaha
Serikali ishughulikie vurugu za kidini
Naungana na Watanzania wenzangu kulaani mauaji ya viongozi wawili wa dini ya Kikiristo yaliyotokea mkoani Geita na mjini Zanzibar, hivi karibuni. Aidha, natoa mkono wa tanzia kwa familia, ndugu na waumini wa dini hizo.
FIKRA YA HEKIMA
Tumeruhusu kucheka na nyani shambani, tutavuna mabua
Ni wazi sasa maji yanaelekea kuuzidi unga! Nchi yetu iko katika hatari ya ‘kuvuna mabua’ kufuatia kasumba ya kutoa mwanya wa ‘kucheka na nyani shambani’. Serikali na vyombo vyake vya dola vitabaki kulaumiwa, kwa kushindwa kudhibiti mfululizo wa matukio ya kutisha yakiwamo mauaji ya watu kikatili.