Category: MCHANGANYIKO
Nashauri kwa hili waanze na Pinda
Haraka haraka baada ya kuanguka kwa jengo lenye ghorofa 16 katika Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam, viongozi wa Serikali wakatoa amri ya kukamatwa kwa Mkandarasi, Mhandisi Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Ukaguzi wa Majengo wa Manispaa ya Ilala.
FASIHI FASAHA
Ulimi mzuri utaimarisha uchumi Tanzania
Juma lililopita nilizungumzia thamani ya faraka ya matumizi ya ulimi wa mwanadamu. Ukitumika vizuri huleta rutuba chanya ya maendeleo, na ukitumika vibaya huleta rutuba hasi ya maendeleo, iwe ya mtu kikundi cha watu ama Taifa.
FIKRA YA HEKIMA
2015 tuwakatae wabunge, mawaziri wa aina hii
Kwa hakika Watanzania hatuna sababu ya kuwarejesha madarakani wanasiasa hawa, kwa vile wametudhihirishia wazi kuwa nia yao ilikuwa ni zaidi ya kutuongoza na kututumikia.
Ninazungumzia wabunge na mawaziri wasiopokea simu za wananchi wa kawaida. Waswahili wanasema kufanya kosa si kosa; kurudia kosa ndiyo kosa.
Waishio mabondeni wahame; wahamie wapi?
Umekuwa wimbo wa kila ufikapo msimu wa mvua za masika, kuwasikia viongozi wa Serikali wakihimiza kwamba waishio mabondeni wahame, kwa vile wanaishi kwenye mazingira hatarishi ya maisha yao na mali zao.
China: Mkombozi pekee uchumi wa Afrika
Historia inazungumza mambo mazuri juu ya Afrika. Inaitaja Afrika kama chimbuko la maendeleo. Binadamu wa kwanza duniani anatajwa kuishi Afrika. Olduvai Gorge iliyopo Arusha nchini Tanzania, inatajwa kama eneo alikoishi binadamu wa kale zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita.
NHC: Hatuhusiki ujenzi ghorofa lililoanguka
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejitokeza na kukana kuhusika na ujenzi wa jengo la ghorofa 16 katika Mtaa wa Indira Gandhi, jijini Dar es Salaam, ambalo lilianguka wiki iliyopita.