JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Utajiri wa Loliondo na laana yake (3)

Sehemu iliyopita, mwandishi alieleza namna watu wa koo za Boroko la Loita kutoka Kenya walivyoingia Loliondo na kuonekana ndiyo wakazi halali wa eneo hilo. Anaeleza pia chanzo cha mgogoro Loliondo akisema ni vita ya uchumi ambayo sasa imepata kasi kutokana na raia wa kigeni na NGOs zinazofadhiliwa na mataifa ya Ulaya na Marekani. Endelea.

Ijue historia fupi ya Nelson Mandela

 

Nelson Rolihlahla Mandela ni Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini ya kidemokrasia. Ni mtu aliyejijengea heshima kubwa duniani kutokana na jitihada zake kubwa zilizofanikisha uhuru wa nchi hiyo na nyinginezo katika Bara la Afrika.

Hofu yatanda uwekezaji Kurasini

. Wanaohamishwa hawajui watakacholipwa

. RC Dar, diwani wawataka wavute subira

. Tibaijuka, Nagu watafutwa bila mafanikio

Hofu ya kuchakachuliwa fidia imetanda miongoni mwa wananchi wanaohamishwa kupisha ujenzi wa Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa katika Kata ya Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Waraka kutoka mtandaoni

Wanaosoma Ujerumani wamlilia Kikwete

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, kwanza naomba niombe msamaha kwa kutumia forum hii badala ya kukuandikia binafsi. Hii ni kwa sababu ya dharura ya jambo lenyewe linalohitaji hakika hatua za haraka sana ili kuokoa haya yanayotokea. Hivyo, naomba unisamehe kwa kuweka bayana hili hapa.

Hongera Kikwete, Membe; Salva rekebisha kasoro hii

 

Julai 1 na 2 zilikuwa siku za pekee katika historia ya Tanzania. Tanzania ilihitimisha kilele cha ugeni mkubwa kuja hapa nchini ndani ya mwaka mmoja. Katika siku hizi taifa lilikuwa na ugeni mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Obama.

 

Afrika inaelekea kutawala uchumi Afrika (1)

 

Nawasalimu wasomaji wote, ninawapongeza na kuwashukuru wote ambao wamekuwa wakiwasiliana nami. Mbarikiwe. Itakumbukwa kuwa huko nyuma nimepata kuandika makala iliyokuwa na kichwa, ‘Naiona Afrika ikiinuka tena’.