Category: MCHANGANYIKO
Chameleon atwaa tuzo ya mwanamuziki bora Uganda
Msanii maarufu wa muziki nchini Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama, Jose Chameleon, hivi karibuni alitwaa tuzo ya msanii bora wa kiume wa kimataifa nchini humo. Chameleon ametwaa tuzo hiyo baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka katika tuzo za Africa Entertainment Awards, zilizofanyika jijini Kampala, hivi karibuni.
Armstrong kurejesha medali IOC
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inamsubiri mwendesha baiskeli wa Marekani aliyepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini, Lance Armstrong, arejeshe medali ya shaba aliyoshinda kwenye mashindano ya Olimpiki ya mjini Sydney, mwaka 2000, amesema Mkuu wa Tume ya Sheria ya IOC.
Hatuiaibishi Mahakama bali tunaijengea uwezo
Wiki iliyopita Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, ametoa taarifa ndefu kwa vyombo vya habari akilishambulia Gazeti la JAMHURI. Mashambulizi ya Jaji Kiongozi yalijielekeza katika msingi kwamba JAMHURI imekuwa ikifuatilia kazi za Mahakama, tena si kwa uzuri bali kwa kutafuta mabaya yanayofanywa ndani ya Idara hiyo.
Messi alipa faini ya kukwepa kodi
Nyota wa timu ya soka ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi pamoja na baba yake mzazi wamelipa euro milioni tano, sawa na dola milioni 6.6 za Marekani, baada ya kubainika na kosa la kukwepa kodi. Messi na mzazi wake huyo walidaiwa kukwepa kulipa kodi hiyo ya serikali kwa njia za ujanjaujanja.
Golikipa mwanamke ashinda tuzo Ujerumani
Golikipa wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Ujerumani, Nadine Angerer, ameshinda tuzo ya mwanamke bora mcheza soka barani Ulaya.
Vitisho vya Mahakama kwa gazeti Jamhuri
Septemba 3, mwaka huu, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Fakihi Jundu, aliitisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam na kutoa taarifa ifuatayo:
TAARIFA YA MAHAKAMA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA NA GAZETI LA JAMHURI; LIKIWATUHUMU WAH; MAJAJI NA MAHAKIMU KUWALINDA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA
Hivi karibuni imekuwa ni kawaida kusikia Majaji, Mahakimu au kesi mbalimbali zilizo mahakamani zikiendelea kusikilizwa, au maamuzi fulani yaliyotolewa na mahakama kulalamikiwa katika vyombo vya habari, na hatimaye watoe maamuzi husika au wasikilizaji wa kesi husika, ambazo nyingine huwa bado zinaendelea mahakamani kudhalilika na kuhukumika, na wakati mwingine, ushahidi kuharibika au kumshawishi Jaji au hakimu kutoa maamuzi kwa kufuata maoni ya magazeti, na ilhali maadili ya kazi za ujaji hayatoi mamlaka kwa walalamikiwa kujibu kwa kukanusha shutuma zilizo mbele yao kwa njia ya vyombo vya habari.
- Simba yaifanyia umafia Dodoma Jiji, yainyuka 6 -0
- Tanzania, Ireland kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo
- Kamati ya Bunge yaridhishwa na utendajikazi wa TPA bandari ya Tanga
- Askari wa Usalama Barabarani Mlandizi watakiwa kuendelea kusimamia vyema sheria
- Watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali watakiwa kuendelea kuzingatia maadili ya utumishi umma
Habari mpya
- Simba yaifanyia umafia Dodoma Jiji, yainyuka 6 -0
- Tanzania, Ireland kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo
- Kamati ya Bunge yaridhishwa na utendajikazi wa TPA bandari ya Tanga
- Askari wa Usalama Barabarani Mlandizi watakiwa kuendelea kusimamia vyema sheria
- Watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali watakiwa kuendelea kuzingatia maadili ya utumishi umma
- DC Kibaha afungua Baraza Kuu la Wafanyakazi Dawasa
- Umeme wa Jotoardhi kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa ifikapo 2030 – Mramba
- Mifumo rafiki ya upatikanaji wa nyaraka iwekwe kuwafikia wananchi kwa wakati
- Almasi, dhahabu yaipaisha Shinyanga, fursa bado zipo njooni – Mapunda
- Urusi yakubali kumaliza vita Ukraine
- Kamati ya Bunge yaridhishwa utekelezaji mradi wa umwagiliaji Nyida, Shinyanga
- Waziri Ndumbaro awashangaa wadhamini wa taasisi wasio na weledi
- Rais ashiriki mkutano wa dharura wa SADC kwa mtandao
- Rais Mstaafu Kikwete aenda Japan kwa ziara maalum yenye lengo la kuimarisha elimu
- Tanzania Kushiriki Maonesho ya Expo Osaka mwezi ujao