JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Huduma mbovu za jamii zitaangusha CCM

Tunapozungumzia huduma za jamii huwa tunazungumzia masuala ya elimu, afya ,maji, umeme, huduma kwa wazee, huduma kwa walemavu na kadhalika.

Majibu kwa porojo za Nyalandu

Asoma na kujibu kiubabaishaji tuhuma kwenye magazeti aliyodai awali kuwa ni ya kufungia maandazi. Kwa muda mrefu sasa baadhi ya magazeti hapa nchini yamekuwa yakiujuza umma ukweli kuhusu Lazaro Nyalandu, ambaye kwa takriban miezi tisa sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii. Habari kumhusu Nyalandu zilianza kutolewa hata kabla hajawa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, wakati angali Naibu Waziri katika Wizara ya Viwanda na Biashara, chini ya Cyril Chami wakati huo. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakati huo alikuwa Joyce Mapunjo.

Balozi Mushi nakuunga mkono, ushoga hapana

Mpendwa msomaji natumaini hujambo kiasi. Nakushukuru wewe na wengine kwa ujumbe na mrejesho mkubwa mlionifikishia wiki iliyopita, baada ya makala yangu ya kuomba Watanzania tusifanye majaribio katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania 9, Desemba, 1978

Ndugu Wananchi,

Leo ni siku ya ambayo Tanzania Bara inatimiza miaka 17 tangu tumejikomboa na ukoloni. Kwa kawaida siku kama ya leo  huwa tunafanya Gwaride Rasmi ambalo huwa lina  linakaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Mwekezaji alivyomvuruga Kamishna Madini

Mwekezaji katika migodi ya madini ya ujenzi, Majaliwa Maziku, anadaiwa kumlaghai Kamishna wa Madini nchini Tanzania, Paul Masanja, ili kufanikisha azma yake ya kupora ardhi ya wananchi kinyume cha sheria ya madini.

Kunani tena kwa Hasheem Thabeet?

Klabu ya Pistons inayoshiriki kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani maarufu kama NBA, imemtema rasmi mchezaji Mtanzania, Hasheem Thabeet, pamoja na nyota wengine wanne.