Category: MCHANGANYIKO
Buriani Mbogora, bado sisi tunahangaika na Malawi
Moyoni nina majonzi. Natumia neno hili kwa vile siamini macho yangu, lakini ndivyo ilivyo. Hili linatokana na kifo cha mwanahabari mwandamizi, Alfred Mbogora. Nilimwona Mbogora siku moja kabla ya kifo chake, lakini zamu hii hakuwa akifahamu kama nilifika kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini angalau alitikisa mkono na mguu nilipoingia wodini. Hii ilikuwa Ijumaa.
Mahakama imekalia haki yangu miaka 16
Mhariri wa JAMHURI nimevutiwa kwa kiwango kikubwa baada ya kusoma toleo lenu Na 39 la Agosti 14-20, 2012 lililoongozwa na habari yenye kichwa kisemacho ‘Majaji Vihiyo Watajwa’. Mara tu niliposoma habari hii, nikaona ni vyema nifunge safari na kuja hapo ofisini kwako nieleze kilio changu. Wengi wa majaji waliotajwa wameshiriki kwa namna moja au nyingine kukandamiza haki yangu.
Hongera Mkapa, Kikwete alijiandalia aibu ya Mahalu
Napata wakati mgumu. Napata shida jinsi ya kuanza makaha haya. Napata shida si kwa sababu nina maslahi binafsi, bali kwa sababu nakumbuka hadithi ya mwanafunzi aliyebeba upodo huku akijifunza kurusha mishale ya sumu. Hakuwa mahiri na hakujua jinsi ya kuvuta upinde. Kwa kicheko kikubwa, aliipaka sumu ncha ya mshale, upinde akauelekeza karibu na tumbo lake, kamba ya kurushia mshale ikatokea mbele yake.
Ni aibu TFF, ZFA kugombea Sh milioni 12 za mgawo wa BancABC
Wiki iliyopita, Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) lililazimika kuutolea ufafanuzi mvutano wa mgawo wa fedha za michuano ya BancABC Super 8 kati yake na Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA), kilipotishia kuziondoa timu zake. Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa fedha zote zilizotolewa na wadhamini wa michuano hiyo – BancABC – zimelipwa kila sehemu kunakohusika zikiwamo timu zote zinazoshiriki, viwanja vinavyotumika, miji inakochezwa na promosheni ya masoko iliyogharimu shilingi milioni nane.
Olimpiki: Kweli kupanga ni kuchagua
Leo nimeazima busara ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyesema kwamba kupanga ni kuchagua.
Uongozi wa Mwalimu Nyerere haujapata kutokea, si Tanzania tu bali katika nchi nyingi za dunia, hata kama katika hili kuna wale wasioambilika. Kama mipango yote aliyokuwa ameisuka na kuanza kutekeleza Mwalimu ingepata wasimamiaji wazuri, nakuapia leo tungeweza hata kuandaa michezo ya Olimpiki.
Yah: Mwongozo wa Spika, lini serikali itahamia Dodoma?
Wanangu, leo ni siku nyingine ya Jumanne katika wiki hii ambayo ni nadra sana kuifikia, kama hujui kwamba kesho ni mtihani mkubwa kwako kutokana na siri kubwa aliyonayo Mwenyezi Mungu juu yako; ni yule ambaye si muumini wa dini yoyote ndiye anayeweza akawa kichaa asijue hilo. Nimefarijika mno na demokrasia inayoendelea hapa nchini kwa mambo ambayo kama si kigezo, yanaweza yakatutoa siku moja hapa tulipo na kutupeleka kule tutakako kwa nia njema na ya dhati kutoka kwa hao waitwao watawala wenye nia njema ya maendeleo.