Category: MCHANGANYIKO
Bomu la Lowassa: Tumeligundua, tunaliteguaje?
Tumeshaelewa hoja ya Edward Lowassa, nadhani sasa ni wakati wa kuelekeza juhudi zetu katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
JK kikwazo CCM
*Yabainika ndiye mwasisi wa makundi CCM
*Akemea dhambi iliyomwingiza madarakani
Staili ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete, inatajwa kwamba haitakuwa na msaada mkubwa wa kuiwezesha Sekretarieti mpya kutekeleza ahadi na maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane uliomalizika mjini Dodoma hivi karibuni.
Yaliyotikisa Mkutano wa Tisa wa Bunge
Mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulihitimishwa Novemba 9, mwaka huu, mjini Dodoma, ukiwa umetikiswa zaidi na hoja binafsi za wabunge; Kabwe Zitto, Halima Mdee na hukumu ya Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Chadema vaa miwani muone CCM walipoangukia
Wiki iliyopita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza mkutano wake wa Nane. Katika mkutano huu kimemchagua Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula na wa Visiwani, Dk. Ali Mohamed Shein, huku Wilson Mukama aliyeingia madarakani kwa kuwapiga fitina viongozi waliomtangulia akienguliwa wadhifa huo alioutumikia kwa miezi 17 tu, na ukatibu Mkuu wa CCM ukatua kwa Abdulrahman Kinana.
Na sisi tuchague makamishna wa polisi
ALHAMISI ya wiki iliyopita shule za msingi zilifungwa, watoto wakabaki majumbani na wazazi wao. Kwenye shule zao na katika vituo vingine mbalimbali, kulikuwa na kazi kubwa ya kisasa ya kuchagua makamishna wa polisi na uhalifu.
Yah: Naikumbuka TBC ya kweli
Wanangu, naamini hamjambo baada ya kupumzika nyumbani na kutafakari maisha yenu ya miaka ijayo na hatima ya kizazi chenu cha dotcom. Sina hakika miaka michache ijayo baada ya dotcom kuzeeka, sijui kutakuwa na kizazi gani?