Category: MCHANGANYIKO
Kiwanda cha Askofu chadaiwa kutiririsha sumu Geita
Kiwanda kidogo cha kuchenjua marudio ya madini ya dhahabu, kilichojengwa kwenye makazi ya watu katika Mtaa wa Kagera mjini Geita, mali ya Askofu wa Kanisa la Habari Njema la Geita, Triphone John, kimesababisha madhara yakiwamo ya kufa kwa mifugo.
Io wapi Simba Arena, ghorofa la kisasa Msimbazi?
Wakati uongozi wa Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club ya jijini Dar es Salaam unaingia madarakani Agosti 2009, ulitoa ahadi nyingi ambazo wanachama waliwaamini na kujenga imani nao.
Kada wa CCM jangili atajwa
Bunge limeambiwa kwamba kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohsin Abdallah Shein, ni mmoja wa majangili wa kimataifa wanaomaliza tembo hapa nchini.
Shein ametajwa na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Peter Msigwa.
Jellah Mtagwa aibua huzuni bungeni
*Ameichezea Stars miaka 15, sasa yu hohe hahe
*Sura yake ilipamba stempu kwenye miaka ya 1980
*Azzan: Ngoja wafe… msome wasifu wao mrefu
Majibu ya Serikali kuhusu kutomsaidia Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Jellah Mtagwa, yamewaudhi baadhi ya wabunge.
KONA YA AFYA
Jinsi kitambi kinavyoathiri nguvu za kiume, afya Unajitazama katika kioo, lakini unachukizwa! Unachukizwa na mwili wako mwenyewe. Huna la kufanya, unabaki kuhuzunika tu. Tumbo! Tumbo! Naam, tumbo lako linaonekana kutuna na kutengeneza mkunjo. Linaonekana linaweza kuchukua muda mrefu…