JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Kashfa zimelilemea Jeshi la Polisi

Wakati fulani wabunge waligombana na aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Omar Mahita. Hoja ilikuwa kwamba Jeshi la Polisi lilistahili kuvunjwa ili liundwe upya. Wakatoa mfano wa Jeshi la kikoloni la King African Rifles (KAR), lilivyovunjwa baada ya maasi ya mwaka 1964 na kuundwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Stars tupeni raha Watanzania

Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) inatarajiwa kushuka dimbani Juni 8 mwaka huu, kucheza na Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Mashindano ya Kombe la Dunia 2014 yatakayopigwa nchini Brazil.

Mbunge Geita adaiwa kuwatapeli walimu mil 11.3/-

Mbunge wa Geita, Donald Max (CCM), ameingia katika mgogoro na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Geita, akidaiwa kukitapeli Sh milioni 11.3.

Mtwara wanadanganywa, maadui wanajipenyeza

Nilidhani nimeandika kiasi cha kutosha katika mada hii, lakini kutokana na msukumo wa wasomaji wa safu hii, na watazamaji wa kipindi cha ‘Jicho la Habari’ kupitia Star TV, nilichoshiriki Jumamosi iliyopita, nimelazimika kuandika tena juu ya mada hii.

Tanzania haiwaamini makocha wa kigeni

Hivi sasa watu duniani wanaonekana kupenda mchezo wa soka zaidi kuliko michezo mingine, na mezzo huo umekuwa ukiongeza ajira kwa vijana kila kukicha.

Yah: Tuliangalie sakata la elimu kwa sasa [2]

Wiki jana nilizungumzia juu ya elimu ya kambo wakati nikihitimisha barua yangu. Nilijaribu kuangalia tofauti za elimu ya sasa na ya zamani japokuwa hazipaswi kufananishwa kutokana na mitaala na manufaa baada ya masomo. Sisi tulifundishwa kujitambua na kujitegemea na ninyi kwa sasa mnafundishwa kutegemea na kutojitambua.