JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

King Majuto: Serikali inisaidie trekta

Hivi karibuni, gazeti la JAMHURI limefanya mahojiano na Amri Athumani, anayejulikana pia kama King Majuto. King Majuto amekuwa mwigizaji wa vichekesho kwa miaka 55 iliyopita. Mtanzania huyu mwenye umri wa miaka 65 anajivunia tasnia ya uigizaji, ila anaomba Serikali imsaidie trekta aweze kushiriki Kilimo Kwanza.

FIKRA YA HEKIMA

 

Mbunge Nyimbo kanena,

Rais apewe kipaumbele

Hivi karibuni, Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Cassian Nyimbo (CCM), alivishauri vyombo vya habari kujenga dhana ya kuzipatia kipaumbele habari za Kiongozi wa Nchi, Rais.

Bila ardhi masikini hawa watakwenda wapi?

Kabla ya kuendelea, niwapongeze viongozi wote wakuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Nampongeza mno Waziri Anna Tibaijuka, na Katibu Mkuu Patrick Rutabanzibwa (PR).

Yah: Tuliangalie sakata la elimu kwa sasa [2]

Wiki jana nilizungumzia juu ya elimu ya kambo wakati nikihitimisha barua yangu. Nilijaribu kuangalia tofauti za elimu ya sasa na ya zamani japokuwa hazipaswi kufananishwa kutokana na mitaala na manufaa baada ya masomo. Sisi tulifundishwa kujitambua na kujitegemea na ninyi kwa sasa mnafundishwa kutegemea na kutojitambua.

FASIHI FASAHA

Watanzania tunakinyanyasa,

tunakibeua Kiswahili – 7

Sina budi kutoa shukrani kwa wale wote walioniunga mkono katika mada hii ya Watanzania tunakinyanyasa na kukibeua Kiswahili. Ni dhahiri Watanzania wanatambua na wanajali lugha yao ya Kiswahili. Asante. Baadhi ya Waswahili wanasema kuwa lugha ya kaya, kabila, rika, masikani na vijiweni, na hata sehemu zetu za kazi, au michezo zisiwe ni vigezo kuwa Watanzania hawakithamini Kiswahili. Hizo ni lugha za msimu tu.

 

FIKRA YA HEKIMA

Wawekezaji wazawa waungwe mkono

Watanzania tumejenga kasumba mbaya ya kuwathamini wawekezaji wa kigeni. Wakati huo huo tumekuwa kikwazo kwa wawekezaji wazawa!