Category: MCHANGANYIKO
Katiba ya Simba inavyompa Rage kifua
Kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club ya Dar es Salaam siku kadhaa zilizopita, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo walitaka kuwapo agenda ya kufanya marekebisho katika baadhi ya vipengele vya katiba ya Wekundu hao wa Mtaa wa Msimbazi.
Yah: Nimechoka na nyimbo zenu sasa
Pamoja na kwamba natukanwa sana na vijana wa dotcom, wakiamini kuwa wako sahihi kwa matusi yao na uhusiano wa kile ambacho nakizungumzia au kukiandika katika waraka huu, najua iko siku nao watakuwa BBC, yaani ‘Born Before Computer’ kwa kizazi chao kitakachokuwa kimekengeuka kuliko wao.
Mzungu afanyiwa tohara ya kimila Afrika Kusini
Kijana wa kiume Mzungu mwenye asili ya Afrika Kusini, amefanyiwa tohara ya kimila nchini humo. Tohara ya kimila katika baadhi ya makabila nchini Afrika Kusini huashiria hatua ya ukuaji kwa kijana inayompatia hadhi ya kuitwa mtu mzima katika familia.
Soka la Tanzania bado lina changamoto
Wakati timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilipopoteza mchezo wake dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wiki iliyopita kwa kufungwa goli 1-0, wadau wa soka walikuwa na mengi ya kusema dhidi ya kipigo hicho.
Tunza sura yako ivutie
Kila mtu anapenda sura yake iwe laini, nyororo ya kung’aa. Wakati mwingine sura zetu huchakaa kutokana na mihangaiko ya hapa na pale. Zifuatazo ni hatua za awali za kutunza ngozi ya sura yako ionekane vizuri.
KAULI ZA WASOMAJI
Biashara vyuma chakavu imulikwe
Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kwamba biashara ya chuma chakavu inafanyika bila leseni, inakwepa kodi, inahujumu miundombinu, inahodhiwa na wageni, inatakatisha fedha chafu, lakini hatua hazijachukuliwa. Ninazidi kuomba chama tawala kitupie jicho kero hii. Haki na amani ni mapacha, na tanzania ni yetu sote.
H.Q. Batamuzi
0782 828 856