JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

JAMHURI YA WAUNGWANA

Mungu tunamtwisha mizigo isiyomstahili

Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, amesema kama kweli Watanzania wanataka kuondoka kwenye lindi la umasikini, waige kile kilichofanywa na nchi yake. Amesema China ya miaka 50 iliyopita ilifanana kwa kila hali na Tanzania ya wakati huo, ambayo imegoma (imegomeshwa) kubadilika. Imeendelea kuwa hivyo hivyo licha ya rasilimali nyingi.

FASIHI FASAHA

Miaka 50 hakuna maendeleo! (1)

Mengi yanasemwa, yanaimbwa na hata kubezwa eti hakuna maendeleo tangu nchi yetu ipate Uhuru wa bendera. Hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana kuinua maisha na mazingira bora ya mwananchi. Mtazamo huo una sura mbili kutokana na asili ya mazungumzo ya watu wanaosema, wanaoimba na wanaobeza. Sura ya maendeleo ya kwenda mbele na sura ya maendeleo ya kurudi nyuma. La msingi nani anazungumza na sababu gani ya kuzungumza.

FIKRA YA HEKIMA

Mishahara mipya isiwe kinadharia

Hivi karibuni Serikali imetangaza viwango vipya vya mishahara kwa watumishi wa umma, vitakavyoanza kutumika mwezi huu, ikitaja kima cha chini kuwa ni Sh 240,000. Mei 29, mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliliambia Bunge kuwa Serikali imekamilisha pia mchakato wa kuongeza kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi kitakachoanza kutumika rasmi Julai 1, mwaka huu.

Yah: Tanzania na maendeleo ya mdomo  

Nianze kwa kuwashukuru sana wazazi wangu walionikanya wakati naoa kwamba maisha ya ndoa ni kama glasi ndani ya kabati, ipo siku lazima kabati litayumba na glasi zitagongana, na ikitokea hivyo katika maisha yangu ya ndoa lazima nitumie kuta nne za chumbani kwangu kumaliza kelele zetu za glasi, ugomvi na sintofahamu yoyote ile.

Extra Bongo wajipanga kutumbuiza Idd

Bendi ya Muziki wa dansi ya Extra Bongo ya jijini Dar es Salaam inajipanga kuhakikisha inafanya maonesho ya kusisimua wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Idd.

Lady Gaga kutumbuiza MTV

Msanii  maarufu  wa muziki wa Pop, Lady Gaga, anatarajiwa kutumbuiza katika tuzo za muziki za MTV zitakazofanyika Agosti, mwaka huu. Litakuwa onesho lake la kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa sehemu za nyonga.