JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Malinzi: Uwanja wa Kaitaba unarekebishwa

Chama cha Soka mkoani Kagera kimewaondoa wasiwasi mashabiki wa mchezo huo mkoani humo kuhusu kasoro za Uwanja wa Kaitaba, kikisema unafanyiwa marekebisho uweze kutumika wakati wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zitakazoanza hivi karibuni Agost 24 mwaka huu.

Mabaraza ya Katiba yadai uhuru wa habari

Leo kwa makusudi nimeamua nijadili mada hii sambamba na mada iliyotangulia hapo juu. Pamoja na matukio yanayoendelea ya uhalifu niliyoyajadili kwa kina kwenye safu yangu ya Sitanii, nimeona yaende sambamba na suala la Haki ya Kupata Habari.

Wakulima wa tumbaku waibiwa kitaalamu

Viongozi wa vyama vya ushirika mkoani Ruvuma, wanatumia hesabu za kisayansi kuwaibia wakulima mabilioni ya shilingi, hali iliyozaa mtafaruku mkubwa. Chama Kikuu cha Ushirika Songea, Namtumbo (SONAMCU) kimesambaratishwa baada ya viongozi kufukuzwa  uongozi katika vyama vya msingi kwa tuhuma ya kuwaibia fedha wakulima wa tumbaku.

Wauza ‘unga’ waanza kutajwa

Wakati Watanzania wengi wakiwa wameamua kuwaanika hadharani nguli wa biashara ya dawa za kulevya, Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo, naye amepasua ukweli wa mambo akisema hali inatisha.

Watu 10,262 wakacha ARVs

 

Watu 10,262 wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi mkoani Mwanza, hawajulikani waliko kwa zaidi ya miezi mitatu sasa baada ya kutohudhuria kliniki ya kutoa dawa hizo.

Tutelekeze wabunge, tuwawezeshe polisi

Wiki hii nimewaza na kuwazua. Kwa furaha nimepokea mrejesho kutoka kwenu wasomaji wangu. Hakika nimefurahi jinsi mlivyolikubali gazeti JAMHURI, na jinsi mawazo tunayoyatoa mnavyoyaunga mkono. Nasema asanteni sana na mkihisi tumekosea, msisite kutusahihisha.