Category: MCHANGANYIKO
Bukoba nani anasema ukweli?
Nchi hii kila kukicha inaacha maswali mengi. Mwanzo niliamua kunyamaza, lakini leo naona ni bora nihoji. Nahoji kutokana na taarifa zinazosambaa na kuzua mgogoro mkubwa ajabu katika mji wa Bukoba. Hapa inadaiwa kuna mapapa wawili – Mbunge Balozi Khamis Kagasheki na Meya Anatory Amani.
Ray C awalaani wauza ‘unga’
Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amewalaani watu wanaofanya biashara ya kuuza dawa za kulevya nchini, akisema wanaharibu maisha ya vijana wengi.
Madudu ya mgodi wa Geita yaanikwa
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kiasi cha Sh bilioni 38.2 tangu mwaka 2007 hadi 2013.
Wakala wa Kaseja kutimuliwa nchini
* Ni yule wa FC Lupopo
Kuna kila dalili kuwa safari ya usajili wa golikipa wa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja, kujiunga na timu ya soka ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kukayeyuka, kufuatia taarifa kuwa huenda wakala wake, Ismail Balanga Bandua, akatimuliwa nchini muda wowote.
Tarime wataja kinachowalazimu kukodisha ardhi kwa Wakenya
Wananchi wa Kata ya Bumera, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, wametaja sababu mbalimbali zinazofanya kuwapo kwa wimbi kubwa la ukodishaji wa mashamba, kwa ajili ya kulima zao haramu la bangi kwa raia wa Kenya.
FASIHI FASAHA
Tusizikwe tungali hai -1
Tusizikwe tungali hai. Nimeanza na kaulimbiu hiyo iliyobuniwa na kutumiwa na wastaafu wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam-(RTD) sasa TBC.