Category: MCHANGANYIKO
Waziri Mukangara, Katibu Kamuhanda sema ukweli wote
Wiki iliyopita wahariri wa vyombo vyote vya habari nchini walikutana mjini Morogoro kujadili mustakabali wa tasnia ya habari nchini. Mkutano huo ulipaswa kufunguliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara. Waziri alikuwa na taarifa zaidi ya miezi miwili. Jumamosi ya wiki iliyopita ndipo akatuma ujumbe mfupi wa simu kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akimweleza kuwa asingeweza kufika.
Jaji Warioba tunatarajia urejeshe Tanganyika yetu – 7
Wiki iliyopita nilichambua kwa kina kifungu cha 32 hadi 46A cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya madaraka ya Rais. Sitarejea niliyoyaandika lakini nashukuru kwa mrejesho mzuri wenye mshindo nilioupata. Wakati toleo hilo linatoka nilikuwa Lushoto mkoani Tanga, kwenye mafunzo yanayohusiana na masuala ya Katiba yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Drogba kamaliza enzi zake Ulaya kwa mafanikio, heshima kubwa
Wiki moja iliyopita, mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba, aliwaaga wachezaji wenzake wa Chelsea baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka minane akitokea Marseille mwaka 2004.
Hujatokwa machozi? Zuru wodi 22
Mapema mwezi huu nimejikuta nikiingia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Hii si mara yangu ya kwanza kufika katika hospitali hii kubwa kuliko zote nchini mwetu.
INAKUWAJE MNAMPA “SHETANI” UMAARUFU? (2)
Wiki iliyopita nilieza kwa sehemu namna wachambuzi na wahubiri wengi wanavyoeleza habari za shetani (Freemason, Illuminat, n.k) katika mitazamo hasi kiasi ambacho hofu imetanda miongoni mwa jamii. Ilivyo sasa ni kuwa watu wengi wamebaki njia panda, hawajui cha kufanya baada ya kugundua kuwa kila wanachokigusa ama kinachowazunguka kimebandikwa hatimiliki ya Freemason ama jumuiya nyingine za waabudu shetani.
Kwa nini watu wanashitakiwa kabla upelelezi haujakamilika?
Moja ya mambo yanayosababisha mrundikano mkubwa wa mahabusu magerezani, ni tatizo la watu kushitakiwa mahakamani halafu wanakosa dhamana au kushindwa kutimiza masharti magumu.