Category: MCHANGANYIKO
Kipande, Magesa wakoroga ICT bandari
Mamlaka ya Bandari Tanzania imegeuzwa sehemu ya ulaji wa hali ya juu. Hata hivyo, kutokana na mtandao mpana wa kuchota fedha unaoanzia wizarani hadi bandarini, yeyote anayetaka kuonesha paka yuko wapi, basi anaishia ama kufukuzwa kazi kwa njia ya vitisho, au kufanyiwa ‘kitu mbaya’.
Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, anamkingia kifua Mkurugenzi wa ICT, Phares Magesa, ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kuzamisha jahazi la bandari Tanzania.
Baada ya kuchapisha sehemu ya kwanza ya matukio yanayoendelea bandarini, wiki hii JAMHURI inakumegea sehemu tu kati ya madudu mengi yanayoendelea bandarini, ambayo kwa kila hali yanadhihirisha kuwa Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, ama hajui kitu kinachoitwa utawala wa sheria, au amedanganywa na watu wanaombeba pale Ikulu, hivyo amepoteza mwelekeo.
Ifuatayo ni sehemu ya barua ya ushauri wa kitaalamu, ambayo ilitolewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi, Mei mwaka jana, akieleza hatari inayoinyemelea bandari kutokana na mfumo wa mawasiliano (Information and Communication Technology – ICT) kuchezewa katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kupoteza mapato, imani ya wateja na kuhatarisha mizigo inayopitia bandarini.
Kwa mshango wa wengi, Dk. Jabir Bakari aliyeandika barua hii na kutoa ushauri, kwa mizengwe tu kama alivyosema Kipande kwenye kikao kati ya Wakurugenzi wa Bodi na Dk. Mwakyembe, Agosti mwaka jana huko Dodoma, kuwa “yeye ni mteule wa Rais na hivyo wakurugenzi hawambabaishi”, Kipande alifanya mbinu Dk. Jabir akafukuzwa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Bandari kwa kutoa ushauri huu. Ifuatayo ni tafsiri isiyo rasmi ya barua hiyo. Endelea…
Kikwete, Warioba wako sawa
Na Christopher Gamaina Wiki iliyopita nchi yetu, Tanzania, iliweka historia ya kipekee. Rais Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza alihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ikiwa ni siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini,…
Bunge la Katiba livunjwe
Wiki hii Bunge linaanza mjadala wa rasimu ya Katiba. Mjadala huu unafanyika siku chache baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwasilisha rasimu hiyo bungeni, na baadaye Rais Jakaya Kikwete naye akalihutubia Bunge. Hotuba mbili za wakubwa hawa ndizo zilizonifanya niandike makala ya leo.
Sitanii, leo tunaumiza vichwa lakini chimbuko la matatizo yote haya liko wazi, ni Rais Jakaya Kikwete. Ibara ya 64 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inasema hivi: “Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar yasiyo mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba itakuwa batili.”
Ibara ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa tangazo la nchi. Inasema Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Zanzibar mwaka 2010 walifanya mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, Ibara ya kwanza ya Katiba ya Zanzibar sasa inasema Zanzibar ni nchi.
Huu ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Tanzania.
Kiwango cha ukiukwaji huu ni sawa na uasi au uhaini.
Ukaushaji sangara kwa moshi ni hatari
* Ni aina ya vibambara, wapakwa mafuta kuvutia wateja
* Wakaushaji wanatumia nguo chakavu, pumba, plastiki
Ukaushaji wa samaki kwa njia ya moshi (kubanika) katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na vitongoji vyake sasa unaanza kuwatia shaka walaji wa samaki hao na wataalamu wa afya.
Walaji wa samaki, hasa wa aina ya sangara (Nile Perch) na sato (Tilapia) ambao wanakaushwa kwa moshi katika Kanda ya Ziwa Victoria maarufu kama vibambara hawatayarishwi katika mazingira salama ya kiafya na mamlaka husika zinaelekea kutokuwa makini katika jukumu la kuhakikisha usafi na usalama wa chakula kwa walaji.
Samaki waliotayarishwa katika mazingira machafu wanadaiwa kuwa kisababishi cha maradhi kutokana na mazingira na vifaa vinavyotumika, ama kuwahifadhi, au kukaushia samaki hao.
Jiji la Mwanza, vitongoji vyake na baadhi ya visiwa vilivyo ndani ya Ziwa Viktoria ni maarufu kwa ukaushaji wa samaki. Kwa Jiji la Mwanza samaki wengi wanakaushwa katika Wilaya ya Ilemela, hasa majumbani na katika baadhi ya fukwe za wavuvi.
Zipo taarifa kwamba utayarishaji wa samaki wa kukausha kwa moshi unaweza kusababisha maradhi kwa watumiaji kama mambo kadha hayakuzingatiwa. Mambo haya ni kama vyombo vinavyotumika, kuwaosha samaki kabla ya kuwasha moto, mahali wanapohifadhiwa tayari kwa kukaushwa, aina ya kuni zinazotumika, muda wa ukaushaji, n.k.
Labda ukaushaji huo ungezingatia utaalamu huenda hatari hiyo ingeweza kuepukika kwa kiasi fulani, lakini uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha ukaushaji wa samaki hao unaofanywa na baadhi ya wauza samaki kwa kiasi kikubwa unafanyika bila kujali afya za walaji.
Sitta maji shingoni
*Hotuba ya Kikwete, kupinda kanuni vyamkaanga *Wapinzani wapoteza imani naye, wadai ni wakala *Wasema Bunge hili ni kikao cha CCM, bora livunjwe Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, ana wakati mgumu. Uchunguzi uliofanywa na Gazeti JAMHURI,…
Katiba mpya Dodoma kama mkutano wa Berlin 1884/85
Ni usiku wa manane. Nimeamka kwa nia ya kuanza safari ya kwenda msibani. Nakwenda Bukoba kuhani msiba wa mama wa rafiki yangu. Huyu si mwingine, bali ni Prudence Constantine, Kaimu Mhariri Mkuu wa Tanzania Broadcasting Corporation (TBC). Machi 2 alfajiri,…