JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Bandari yaishitaki JAMHURI, Mhariri

*Kipande adai fidia Sh bilioni 5.85, aomba lizuiwe kuiandika Bandari

*Mahakama yasitisha kumfukuza Mkurugenzi, Njowoka kushitakiwa

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mzee Madeni Kipande (58) na mtu aliyejiita Katibu wa Shirika la TPA, Christian Chiduga, kwa pamoja wamelifungulia kesi Gazeti Jamhuri mahakamani na Mhariri Mtendaji, Deodatus Balile, wakidai fidia ya Sh bilioni 5.85.

Pia wawili hao walifungua kesi nyingine Mahakama Kuu chini ya Hati ya Dharura mbele ya Jaji Sheikh iliyotarajiwa kuitishwa Jumatatu jana, wakiomba Mahakama itoe amri ya zuio kwa JAMHURI isiendelee kuandika habari zinazohusu Bandari.

Lembeli: Mbunge mahiri au muuza nchi?

Vyombo kadhaa vya habari vimeandika taarifa za Mjumbe wa Bodi ya African Parks Network (APN), James Lembeli, kuwashitaki wanahabari na wahariri wa vyombo kadhaa vya habari.

Kwenye orodha hiyo, jina la Manyerere Jackton limo. Pamoja nami, kuna makomredi wengine walioamua kwa haki kabisa kusimama kidete kulinda rasilimali za nchi yetu. Wito wangu kwa wote — tusikate tamaa.

Hadi naandika makala haya, sijapokea barua yoyote kutoka, ama kwa Lembeli au katika Mahakama ikinieleza bayana suala hilo. Kwa sababu hiyo, bado taarifa hizi nazichukulia kama taarifa nyingine zisizo rasmi, ingawa lisemwalo lipo, na kama halipo, laja.

Ujumbe wa Pluijm uzingatiwe

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Hans Van Der Pluijm, ametema nasaha nzito kwa timu hiyo, ambazo zinastahili kuzingatiwa pia na klabu nyingine za soka hapa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya kumuaga…

Mameneja Tanesco wanolewa kuhusu Mazingira

Kutokana na upungufu wa umeme unaoikabili nchi yetu ya Tanzania, tunategemea kuwa uwekezaji katika sekta ya nishati utaongezeka, hivyo kuibua changamoto nyingi za kimazingira, kiuchumi na kijamii.

Haya yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira Wizara ya Nishati na Madini, Gedion Kasege, hivi karibuni wakati akifungua semina ya siku tano iliyowahusisha mameneja wa Tanesco nchini ili kujifunza masuala ya uhifadhi wa mazingira  (Strategic Environmental Impact Assesment), utwaaji wa ardhi, Sheria ya Mazingira na masuala ya jinsia katika sekta na jinsi ya kukabiliana nayo kuweza kufikia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Tukatae ukatili dhidi ya albino (2)

Juma lililopita nilizungumzia chimbuko na dhana potofu zinazoendelea miongoni mwa jamii yetu kuhusu watu wenye ualbino.  Leo naangalia masuala ya utu, afya, haki, matatizo na usalama wao.

“Watu wenye ualbino” kama wanavyotaka wao wenyewe kuitwa, na wasiitwe albino au zeruzeru kwa sababu majina hayo yanadhalilisha utu wao. Binafsi sioni kama kuna udhalilishaji juu yao.

Maneno hayo mawili ya Kiswahili na Kiingereza yote yanatoa maana ile ile moja ya kukosa rangi kamili ya mwili. Ni vyema ndugu zangu wayakubali majina hayo. Nasema ninawaomba wayakubali majina hayo.

Ugaidi Kenya utuimarishe kiulinzi

 

Wimbi la matukio yanayohusishwa na ugaidi limeendelea kuitesa nchi ya Kenya kwa kuua na kujeruhi watu, kuharibu mali mbalimbali na kuisababishia hasara kubwa.

Wiki iliyopita watu zaidi ya 10 waliripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa wakati wa milipuko miwili iliyotokea katika soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi.

Huo ni mfululizo wa matukio kadhaa yanayohusishwa moja kwa moja na ugaidi likiwamo lililoshambulia kituo cha maduka ya kifahari cha Westgate jijini Nairobi.